Kulia ni Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais, Mazingira, Dokta BINILITHI MAHENGE na Meneja wa Kanda za juu kusini wa Airtel bw, Straton Mushi na baadhi ya wanafunzi wa shule ya sekondari iwawa wakifurahia baadda ya hafla ya makabidhiano ya msaada wa vitabu vyenye thamani ya shilingi milioni 15 utakaofaidisha jumla ya shule 5 zilizopo wilaya ya Makete mkoani Njombe. Shule zinazofaidika ni Iwawa, Kipagalo, Mlondwe, shule ya Makete ya wasichana na ile ya Ipelele zote mkoani Njombe wilaya ya Makete. Hafla ya makabidhiano ilifanyika jana katika shule ya Iwawa iliyopo wilayani Makete.
Kulia ni Meneja wa Kanda za juu kusini wa Airtel bw, Straton Mushi akikabidhi msaada wa vitabu kwa Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais, Mazingira, Dokta BINILITHI MAHENGE utakaofaidisha jumla ya shule 5 zilizopo wilaya ya Makete mkoani Njombe. Shule zinazofaidika ni Iwawa, Kipagalo, Mlondwe, shule ya Makete ya wasichana na ile ya Ipelele zote mkoani Njombe wilaya ya Makete. Hafla ya makabidhiano ilifanyika jana katika shule ya Iwawa iliyopo wilayani Makete. Anaeshudia kushoto ni mkuu wa shule msaidizi bw, Fadhili Dononda.

Mradi wa SHULE YETU unaotekelezwa na Kampuni ya Simu za Mkononi ya AIRTEL umeendelea kunufaisha shule kadhaa nchini kwa sasa umeingia wilayani Makete, Mkoani Njombe na kutoa msaada wa Vitabu vya kiada na ziada vya masomo ya sayansi vyenye thamani ya shilingi zaidi ya Milioni 15 kwa shule tano wilayani humo.

Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais, Mazingira, Dokta BINILITHI MAHENGE ndiye aliyepokea shehena ya Vitabu hivyo ambapo pamoja na mambo mengine amesifu Msaada huo kuwa unaunga mkono Juhudi za Rais JAKAYA KIKWETE katika kufanya mabadiliko makubwa katika sayansi na teknolojia nchini kwa kuwekeza kwenye elimu.

Hafla fupi ya makabidhiano ilifanyika katika viwanja vya shule ya sekondari ya Iwawa iliyopo wilayani Makete Mkoani Njombe kwa niaba ya shule zingine zinazofaidika na mradi huo zikiwemo Kipagalo, Mlondwe, shule ya Makete ya wasichana na ile ya Ipelele zote mkoani Njombe wilaya ya Makete.

MENEJA BIASHARA AIRTEL KANDA YA NYANDA ZA JUU KUSINI STRATON MUSHI alisema "Kampuni ya AIRTEL tunakabidhi vitabu vya masomo ya KEMIA, FIZIKIA na HESABU ikiwa ni mwendelezo wa kuunga mkono juhudi za serikali za kuhamasisha wanafunzi kupenda zaidi masomo ya mchepuo wa sayansi ambapo vyote hivi vinathamani ya shilingi milioni kumi na tano"
Akipokea msaada huo Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais anayeshughulikia mazingira Dr BINILITHI MAHENGE ameipongeza AIRTELL kwa kuungana na Rais JAKAYA KIKWETE aliyethubutu kufanya mabadiliko kwenye masomo ya sayansi.
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: