Kocha Mkuu wa Taifa Stars, Mart Nooij (kulia) akisalimiana
na kocha wa Benin, Didier Olle Nicolle wakati kabla ya kuanza kwa mchezo wa Kimataifa wa Kirafiki uliofanyika kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam. (Picha: Francis Dande na Othman Michuzi)
Kikosi cha Taifa Stars kikiwa katika picha ya pamoja kabla ya pambano lao na Benin.
Mrisho Ngasa akiwatoka wachezaji wa Benin.
Mshambuliaji wa timu ya Soka ya Tanzania, Taifa Stars,
Mrisho Ngasa (kulia) akichuana na beki wa Benin, Adeoti Jordan katika mchezo wa Kimataifa wa Kirafiki uliofanyika kwsenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam. Stars ilishinda 4-1.
Beki wa Stars, Shomari Kapombe akimtoka mchezaji wa Benin, Djigla David.
Mshambuliaji wa timu ya Taifa Stars,Juma Luizio akiipachikia bao nne timu yake katika mtangange wa kikataifa wa kirafiki dhidi ya Benin,uliomalizika hivi punde katika uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.Taifa Stars imeshinda 4-1 dhidi ya Benin.
Wachezaji wa Taifa Stars,wakishangilia ushindi wao huku wakiwaacha wapinzani wao wa Benin wakiwa hoi tena wakiwa hawaamini wanachokiona uwanjani hapo.
Washabiki wa Taifa stars wakiisapoti vilivyo timu yao.
Ubao wa ulionyesha hivi kabla jamaa hawajapata la kufutia machozi.
Shangwe tupu ilikuwa uwanjani hapa.
Toa Maoni Yako:
0 comments: