Mkurugenzi wa Lino International Agency ambao ni Waandaaji wa mashindano ya Urembo ya Miss Tanzania,Hashim Lundenga (kati) akiongea na waandishi wa habari (hawapo pichani) juu ya sakata la umri halali wa Mrembo alietwaa taji hilo Mwaka huu, Sitti Abbas Mtemvu (kushoto),katika mkutano huo Lundenga alitolea ufafanuzi swala la umri wa Mrembo huyo kulingana na vilelezo alivyopewa na mrembo huyo wakati akijiunga na mashindano hayo.
"Katika mashindano ya yetu,Washiriki wote hujaza fomu maalum zilizoandaliwa na Kamati ya Miss Tanzania,katika fomu alizojaza mrembo wa Miss Tanzania 2014 Sitty Abbas Mtemvu amejaza tarehe yake ya kuzaliwa ambayo ni Mei 31,1991 na hivyo kuwa ni sahihi kushiriki mashindano yetu" Alisema Lundenga mbele ya wanahabari hao.

Lundenga aliendelea kusema kuwa Mashindano ya Miss Tanzania hayaruhusu mshiriki yeyote mwenye mtoto kushiri,hivyo katika swala la Sitti Mtemvu kuwa ana mtoto,hilo kalina ukweli wowote bali ni uvumi tu wa kwenye mitandao ya kijamii baada ya Mrembo huyo kuonekana akiwa katika picha na mtoto alieomba kupiga nae.
Hiki ndiyo cheti...
Cheti cha Miss Tanzania 2014, Sitti Mtemvu.
Katika Hali isiyo ya Kawaida leo Mkurugenzi wa Rino International Agency ambao ni Waratibu wa mashindano ya Urembo ya Miss Tanzania Hassim Lundenga ameshndwa kujibu maswali ya waandishi wa habari pale alipoanza kujikanyaga wakati akifafanua juu ya kashfa za zinazomkabili Miss Tanzania 2014 Sitti Abbas Mtemvu.

Akizungumza na Waandishi wa Hababari jijini Dar es Salaam leo Oktoba 21, 2014 Lundenga alisema kuwa wao si wapelelezi wa jambo lolote ambalo linazungumziwa katika mitandao juu ya mambo mbali mbali yaliyokuwa yakizungumzwa, naanza kusema Sitti hana elimu ya Masters hilo la masters sijui mtatoa wapi???

Lundenga amejikanyaga mwanzo mwisho wakati wa mkutano hio hali iliyopelekea kunyesha mwenye majinzi huku watu wakitafsiri kuwa anawadanganya waandishi...

Jambo lingine ambalo limewasikitisha waandishi ni jinsi Miss Tanzania 2014 Sitti Mtemvu alipojikanyaga kanyaga kujibu maswali na kusema kuwa yeye hayupo tayari kuzungumzia lolote na hayo yote mliyoyazungumzia ni uongo na mengine maisha yake binafsi.
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: