MSANII wa muziki wa kizazi kipya nchini, Sunday Mangu ‘Linex’ amesema kuwa hana sababu ya yeye kutumia kilevi chochote kile kama madawa ya kulevya na bangi kwani haoni kama vinaweza kumsaidia katika muziki wake.

Akizungumza jijini Dar es Salaam jana, Linex alisema kuwa yeye hataki kufuata mkumbo kama wasanii wengine wanavyo fanya anachotaka ni kufanya kazi zake ili aweze kuelimisha jamii inayomzunguka na si vinginevyo.

Alisema kuwa hataki kujihusisha na vitendo vya ajabu kwani yeye yupo kwa ajili ya kuelimisha jamii na si kupotosha kwa kufanya vitendo vya ajabu.

“Kiukweli mie sijihusishi na bangi wala madawa ya kulevya ya aina yeyote mimi ni msanii ninayejielewa na siitaji kufanya hivyo kwani nitapoteza mashabiki wanaozidi kunizunguka,”alisema

Aliwataka mashabiki wake wasiwe wanasikiliza maneno yanayoongelewa na watu kwani yeye ni msanii ambaye yupo kwa ajili ya kuelimisha jamii yake inayomzunguka na si vinginevyo.
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: