Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akisalimiana nabaadhi ya viongozi wa dini ya Kikristu, wakati alipowasili kwenye Uwanja wa CCM Kirumba jijini Mwanza leo, Oktoba 19, 2014, kwa ajili ya kuhudhuria sherehe za kuwekwa Wakhfu Askofu Mteule wa Kanisa la African Inland Dayosisi ya Mwanza, Mchungaji John Bunango, iliyofanyika jijini humo leo mchana.
 Maaskofu wakimwekea mikono ya Baraka Askofu mwenzao, Askofu Mteule wa Kanisa la African Inland Dayosisi ya Mwanza, Mchungaji John Bunango, wakati akiwekwa Wakhfu katika sherehe zilizofanyika kwenye Uwanja wa CCM Kirumba jijini Mwanza leo.
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal,
akiwahutubia waumini wa dini ya Kikristu, waliohudhuria katika Sherehe za kuwekwa Wakhfu Askofu Mteule wa Kanisa la African Inland Dayosisi ya Mwanza, Mchungaji John Bunango, zilizofanyika kwenye Uwanja wa CCM Kirumba jijini Mwanza, leo.

 Wanakwaya wakitoa burudani wakati wa sherehe hizo..
 Makamu wa Rais wa Jamhuri wa Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal,
akimpongeza Askofu Mteule wa Kanisa la African Inland Dayosisi ya Mwanza, Mchungaji John Bunango, baada ya kuwekwa Wakhfu katika sherehe zilizofanyika kwenye Uwanja wa CCM Kirumba jijini Mwanza leo.
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya viongozi wa dini ya Kikristu na wanafamilia
ya Askofu
  Mteule wa Kanisa la Africa Inland Dayosisi ya Mwanza, Mchungaji John Bunango, baada ya sherehe za kuwekwa wakhfu zilizofanyika kwenye Uwanja wa CCM Kirumba jijini Mwanza leo.
 Makamu wa Rais wa Jamhuri wa Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal,
akiagana na
  Askofu Mteule wa Kanisa la African Inland Dayosisi ya Mwanza, Mchungaji John Bunango, wakati akiondoka Askofu huyo kuwekwa Wakhfu katika sherehe zilizofanyika kwenye Uwanja wa CCM Kirumba jijini Mwanza leo.
Makamu wa Rais wa Jamhuri wa Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiagana na  baadhi ya viongozi wa dini ya Kikristu wakati akiondoka kwenye uwanja wa CCM Kirumba, baada ya kuhudhuria sherehe za kuwekwa Wakhfu Askofu Mteule wa Kanisa la African Inland Dayosisi ya Mwanza, Mchungaji John Bunango, leo.
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: