Masikini Akipata Matako Hulia Mbwata, bwana mdogo Diamond mtoto wa Tandale ambae wakati Wema Sepetu anakuwa miss yeye alikuwa anauza mitumba kule Tandale
kapata pesa sasa naona makalio yake yanalia Mbwata. 

Kama unampenda sana Diamond usipanic endelea kusoma utanielewa tu Diamond amewakera mashabiki ndio maana yamemkuta yale yaliomkuta pale Leaders. Kijana Diamond alikuwa moja kati ya watu masikini sana nchini, alikuwa ANALALA kwenye mazingira magumu ila leo amediriki kusema kuwa MBEYA HAKUNA HOTELI YENYE HADHI YAKE, hahahaa inachekesha sana. 

Anasahau kuwa umaarufu wake umekuja kwasababu mashabiki WALIAMUA kumkubali. Wema Sepetu wakati ana make headlines akiwa Miss Tanzania hakuwa anatambua kuwa pale mitaa ya Tandale kuna kijana anaitwa Nassibu anauza mitumba, na ninaamini hata kama angeonana na Diaond kipindi kile HAKIKA asingemuangalia mara mbili. 

Ila dogo leo kapata hela anaanza kuleta dharau kwa mashabiki. Dogo ana kauli chafu sana, anapenda kujikweza. Ukitaka ufanikiwe na ufaidi kuwa msanii bongo hakikisha UNAWAFURAHISHA mashabiki wako mdogo wangu. Waache watu wakusifie wewe. Kitu ambacho hujui ni kwamba hapa bongo kulikwa na wasanii wakubwa kama akina Mr. Nice lakini walilewa sifa na sasa wanaishia kucheza pool pale Sinza Ambiance na kutia huruma. 

Usipoangalia wewe na kaka yako Nice mtaakaa kijiwe kimoja na kusema ZAMANI NILIKUWA MAARUFU. Diamond umekuwa na tabia ya kusema wewe ni maarufu na kukataa mara kadhaa (HATA UKIOMBWA) kufanya show sehemu mbali mbali, unajiona ni msanii wa kufanya SHOO ZA MIL 30, kuna cases kadhaa za wewe kuwatolea nje mashabiki kufanya show eti kwa madai unataka hela nyingi. 

Unasahau watanzania hawa hawa ndio waliokupigia kura ukapata hizo tuzo na kuwa nominated hata kwenye hizo BET, lakini naona sasa UMEUCHOKA umaarufu wako na uko tayari kuupoteza kwa upuuzi tu usio wa maana.

Kuna mambo mengi sana unakosea kama binadamu ila kuna mengi unayafanya makusudi kwasababu wewe ni LIMBUKENI, kwa mfano suala la kutoka na mabinti kadhaa wa kadhaa kwako umeona kama ni ufahari hivi, kumbe wenzako wanakuona zuzu tu cuz huwezi kuwamaliza mabinti wote duniani. Na kwasababu hiyo ndio maana wanaume wenye akili WAMEMUHONGA WEMA GARI wakasingizia kuwa ni Kadinda ndiye aliyetoa, ukiacha dharau watu watakuheshimu.

Sijui niendelee au niishie hapa?! Aah nikiishia hapa nitakuwa nimekuogopa. Mdogo wangu wewe kimziki sio kwamba uko juu sana kuliko Alikiba, Linex, Barnaba, Ben Paul au hata Lady Jaydee ni kwamba umepata promo nyingi sana kiasi cha mashabiki KUAMUA kukukubali.

Unashangaa watu pale Leaders Club jijini Dar waliamua kukuzomea ni kwasababu Watanzania wamechoka na majivuno yako na dharau. Sasa T.I anataka kufanya collabo na Ali Kiba ile inaonyesha dhahiri kuwa wewe BADO. Anyways kama umemaindi poai la hayo ni maoni yangu kama SHABIKI na ungekuwa wewe ni chama cha siasa hakika leo ningerudisha kadi yangu ya Uanachama mpaka pale utakapojirekebisha!

Usije ukakonda bure kwa makavu haya. La mwisho Gwanda zile zitakuletea matatizo, inawezekana ulionywa hukusikia jaribu tena uone cha mtema kuni. Next time hutaitwa Oysterbay watakuficha wenye nazo!

Kwa Leo nimemalizia.

Ni mimi Msema Ovyo;
Blasio Kashesha wa Kasuru - Kigoma.
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

2 comments:

  1. Tatizo la wasanii wetu wa TZ wanaona milioni 30 ni hela nyingi sana hizo millioni 30 ukizi convert kwa dola ni pesa ndogo sana. Kumpata Jay Z au Beyonce ni dola 3,000,000 sasa hiyo inaonyesha tofauti ya kijana Diamond na wasanii wanaojulikana duniani. Ushamba ndio unafanya watu wapige picha mbele ya magari mazuri ambayo hata sio yao ili waonekana wana uwezo, hivyo vi gari vya mtumba vinavyotoka Dubai ndio utajiri? Je ukiendesha Lamborghini Murcielago, Ferarri au Porche Cheyenne si ndio hutamsalimia Mtanzania yeyote? Kuhusu na wanawake hata sielewi mentality ya huyu kijana, kwani kutembea na kila msichana ndio sifa? Mimi naona ni sifa za kijinga sijaona mwanaume yeyote aliyenufaika au kupewa shahada sababu ametembea na kila msichana. Nilikuwa LA kwenye tamasha la BET lakini sina haja ya kumtangazia kila mtu nikaona Diamind kapiga picha na Nelly na wasanii wengine basi Blogs zetu zikaandika kuwa wasanii wote walikuwa wanamfuata kuwa yeye ndio alikuwa superstar please give me a break lazima uelewe kuwa wasanii wa Marekani ni very "Humble" hawana najidai wanasalimiana na kila mtu ndio maana utaona kuna wakati wanafanya hata show za bure kuwashukuru mashabiki wao. The bottom line is watu wenye pesa hawana maringo ila watu wenye vijisenti ndio wanataka kila mtu ajue kuwa wana pesa. Pesa sio kitu kikubwa sana kwa watu wenye pesa nyingi a good example ni watu kama Mengi, Bahresa na wengineo ambao wanaongea na kila mtu bila ya dharau. Simjui vizuri Diamond na sitaki kum judge ila hata kama ana pesa, zinamsaidia mwenyewe na usiringie watu wanaolipa kiingilio kuona show zake maana wakiamua kutokuja kwenye show zake utarudi kule kule kwenye kuuza mitumba.

    ReplyDelete
  2. Acheni wivu wa kike...kosa lake ni kujua thamani yake...Kama unaweza basi anaweza

    ReplyDelete