Hali ya Askari wa usalama barabarani, aliyejulikana kwa jina la Riziki, WP 2806 Cpl Riziki, aliyegongwa na daladala aina ya DCM wakati akiwa katika harakati za kutimiza majukumu ya kazi eneo la Mbagala Rangi Tatu, hali yake inaendelea vizuri.

Kwa mujibu wa Askari ambaye hakupenda jina lake litajwe aliiambia Kajunason Blog kuwa afande huyo anapatiwa matibabu hospitali ya Muhimbili na hali yake inaendelea vizuri.

"Mimi nimetoka kumjulia hali, kwakweli alikuwa amepoteza fahamu ila kwasasa anaendelea vizuri maana alikuwa ameshazinduka,"alisisitiza Askari huyo ambaye hakutaka jina lake litajwe.
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: