Mkuu wa mkoa wa Dodoma Dkt Rehema (kati) akikatata utepe kuashiria kulizindua rasmi duka la Airtel Dodoma lililopo barabara ya Mkuu mkoani humo, anaeshuhudia wakwanza kulia ni mkurugenzi wa airtel huduma kwa wateja Bi, Adriana Lyamba na Meneja biashara wa Airtel Dodoma Bw, Stephen Akyoo wakwanza kushoto, Airtel imefanya uzinduzi wa duka hilo jana baada ya kuzindua maduka mengine katika mikoa ya Dar es Salaam, Arusha Mwanza Mbeya na Mtwara. Maduka mengine ya Morogoro, Bukoba na Zanzibar pia yanatarajiwa kuzindulia mwezi huu.
Meneja mauzo wa Airtel Mkoa wa Dodoma Bw Stephen Akyoo akiwa na wafanyakazi wengine wa Airtel Dodoma akitoa maelezo mafupi kwa Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Dr Rehema Nchimbi kuhusiana na muonekano wa duka jipya la Airtel Dodoma lililopo barabara ya Mkuu muda mfupi kabla ya mkuu wa mkoa huyo kuzindua duka hilo jana.
Kati kati ni Mkuuu wa mkoa wa Dodoma Dkt Rehema nchimbi akiwa na Mkurugenzia wa huduma kwa Mteja Airtel Bi Adriana Lyamba (shoto) na Meneja wa Duka hilo mkoani hapo Bi Elida kulia wakikata keki iliyoandaliwa maalum kwa ajili ya uzinduzi wa duka jipya la Airtel mtaa wa Mkuu mjini Dodoma jana.
Mkuu wa mkoa wa Dodoma Dkt Rehema Nchimbi akiongea na wananchi na wanahabari hawapo pichani wakati wa uzinduzi wa duka jipya la Airtel mkoani Dodoma barabara ya mkuu Jana, Airtel ilizindua duka hilo kwa dhumuni la kuendelea kutoa huduma bora kwa wateja wake nchini.
Wafanyakazi wa Airtel mkoa wa Dodoma wakiwa kwenye picha ya pamoja mara baada ya Airtel kufungua Duka jipya mkoani hapo mtaa wa Mkuu jana.

Kampuni ya simu za mkononi ya Airtel imefungua duka lake la Dodoma kufatia  ukarabati uliokuwa unafanyika wa kuliweka duka hilo kuwa la kisasa zaidi ili kuweza kuendelea kuwapatia wateja wake huduma bora zaidi. 

Uzinduzi wa duka hilo ulifanywa na mkuu wa mkoa wa dodo dkt Rehema Nchimbi ambapo amewapongeza Airtel kwa mpango kabambe wa kuboresha maduka yake nchini pamoja na duka la Dodoma.

Akiongea wakati wa uzinduzi huo Mkurugenzi wa Kitengo cha Huduma kwa wateja Bi Adriana Lyamba alisema,"Leo tunazindua rasmi duka hili lenye muundo mpya lililopo katika barabara ya Mkuu hapa Dodoma ikiwa ni moja kati ya mikakati yetu ya kuongeza ufanisi katika utoaji wa huduma zetu na
kupunguza msururu wa wateja wanaoingia dukani hapa kupata huduma
mbalimbali.

Kwa kupitia duka hili wateja wetu watafurahia huduma zetu za pesa mkononi  za Airtel Money ,internet na kuweza kununua muda wa maongezi pamoja  bidhaa zikiwemo simu za mkononi na vifaa vya huduma za mawasiliano na  huduma nyingine nyingi.

Sasa wateja wetu wanauhakika wa kupata huduma bora kwa haraka zaidi kupitia duka hili. Tutaendelea kutoa huduma za kibunifu zenye uhakika na zenye ubora wakati wote kupitia mtandao wetu bora na mpana ulioenea zaidi nchini. Lengo letu ni kuhakikisha tuwapatia wateja wetu uzoefu tofauti
katika huduma zetu na kufikia matarajio yao. aliongeza Lyamba.

Kwa Upande wake Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Mh, Dkt Rehema Nchimbi alisema"  nawapongeza sana Airtel kwa juhudi hizi za kuboresha utoaji wa huduma za mawasiliano kwa watumiaji nchini. Sote tunatambua mawasiliano ni nyenzo muhimu katika kuunganisha jamii na kuendesha shughuli za kibiashara na kiuchumi nachukua fulsa hii kuwaomba wakazi wa Dodoma watumie vyema nafasi hii kupata huduma bora zitakazorahisisha uendeshaji wa Shughuli zao mbalimalbali za kila siku".
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: