Baadhi ya warembo wanaoshiriki Shindano la Redd's Miss Kinondoni 2014 wakiwa katika picha ya pamoja.

Na Mwandishi Wetu.

SHINDANO la Redds Miss Kinondoni linatarajia kuwashusha jukwaani warembo 20 watakaowania taji hilo litakalo fanyika Agosti 15, mwaka huu katika Ukumbi wa Escape 1, Mikocheni Dar es Salaam.

Akizungumza na waandishi wa habari jana, Mratibu wa Shindano hilo, Innocent Melleck, alisema warembo hao tayari wameiva na kinachosubiriwa ni kesho tu kujua mshindi ni nani kati yao.
“Kinachosubiriwa ni siku tu kwani warembo hao wataondoka na zawadi za kila aina na za kuvutia, pia kuna burudani mbalimbali ikiwemo Malaika Band wakiongozwa na Christian Bella pamoja na msanii wa kizazi kipya Young Suma watapagawisha mashabiki” alisema.

Melleck alisema, taji la Redd’s Miss Kinondoni kwa sasa linashikiliwa na Lucy Tomeka, ambaye naye alivikwa na aliyekuwa Redd’s Miss Tanzania, Brigitte Alfred.

Warembo wanaoshiriki shindano hilo wanatoka vitongoji vya Sinza, Msasani na Dar Indian Ocean, huku kiingilio kikitarajiwa kuwa Sh 10,000 kwa viti vya kawaida na Sh 30,000 viti maalumu na watu mia moja wa kwanza kununua tiketi mlangoni kupata Redd’s Original moja ya bure kabisa.
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: