Mmoja wa wachekeshaji mahiri kutoka nchini Tanzania, Mc Pili Pili akielezea jambo kwenye mkutano wa Wanahabari uliofanyika mapema leo jijini Dar, wa pili shoto ni Mkurugenzi Mtendaji wa kituo cha Radio 5, Robert Francis, ambao ndio waandaaji wa Onesho hilo la vichekesho.
Mchekeshaji Fred Omondi kutoka nchini Kenya akiongea machache mbele ya waandishi wa habari katika mkutano uliofanyika leo jijini Dar es Salaama ikiwa ni maandalizi ya onyesho la kesho Agosti 2, 2014. Pembeni yake ni Mchekeshaji Mahiri kutoka nchini Uganda, Anne Kansiime, Mkurugenzi Mtendaji wa kituo cha Radio 5, Robert Francis pamoja na mchekeshaji mahiri kutoka nchini Tanzania, Mc Pili Pili . 
 Pichani wa pili kulia ni Mchekeshaji Mahiri kutoka nchini Uganda, Anne Kansiime akifafanua jambo mbele ya Waandishi wa Habari kuhusiana na burudani yake kubwa atakayoinyesha hapo kesho siku ya Jumamosi kwa mashabiki wake katika ukumbi wa Golden Tulip, jijini Dar.
 Wanahabari wakifuatilia mkutano huo.
 Mkurugenzi wa Kajunason Blog, Cathbert Angelo akipata ukodak na mchekeshaji Anne Kansiime.
  Mkurugenzi wa Kajunason Blog, Cathbert Angelo akipata ukodak na wachekeshaji Mc Pili Pili wa Tanzania (Kushoto) na Fredy Omondi wa Kenya (kulia).
---
Na Mwandishi Wetu.

Mchekeshaji Anne Kansiime toka nchini Uganda anatarajiwa kutoa burudani kubwa siku ya Jumamosi kwa mashabiki wake katika ukumbi wa Golden Tulip.

Akizungumza na waandishi wa habari katika jijini Dar es Salaam, mkali huyo wa kuchekesha na sanaa za majukwaani amesema mashabiki wake watarajie mambo makubwa hapo Jumamosi.

‘Hii ni mara yangu ya kwanza kuja Tanzania, hivyo mashabiki wangu watarajie burudani ambayo itaacha mbavu zao hoi, lakini pia watapata nafasi ya kujifunza vitu vingi kupitia vichekesho vyangu’ alisema Anne.

Kwa upande wake, mchekeshaji mwingine kutoka Kenya atayetoa burudani, Fredy Omondi, amesema watanzania watarajie burudani kali kama lilivyo jina la burudani yenyewe, Cheka Kwa Nguvu.

‘Usiku wa Jumamosi utawakutanisha moja ya wachekeshaji mahiri barani Afrika, hivyo watanzania waje kwa wingi kushuhudia burudani hii’ alisema Fred.

Naye mchekeshaji Pilipili kutoka Tanzania amesema usiku wa leo utakuwa usiku wa kukumbukwa hasa kwa vichekesho alivyowaandalia mashabiki wake.Usiku wa Cheka Kwa Nguvu unaandaliwa na kituo cha Radio 5 na pia utaambatana na burudani ya muziki kutoka ODAMA Band.

Akizungumzia tukio hilo, Mkurugenzi Mtendaji wa kituo cha Radio 5, Robert Francis amewataka wapenzi wa burudani ya vichekesho kuhudhuria kwa wingi ili wafurahie burudani waliyowaandalia.  ‘Usiku huo utakuwa ni maalumu kwa watanzania kufurahia Utanzania wao, kwani kucheka ni sehemu muhimu kwa maisha ya mwanadamu’ alisema Robert.

Kansiime amejipatia umaarufu kupitia mitandao ya kijamiii ambako alianza kwa kuweka vipande vya video akiigiza kama mwanamke wa kiafrika anayekutana na changamoto mbalimbali za maisha.

Mchekeshaji huyo wa kike, ambaye pia huendesha kipindi cha “Don’t Mess With Kansiime” kwenye kituo cha Citizen TV, anatajwa kuwa mwanamke mwenye kipaji cha pekee nchini Uganda na Afrika Mashariki kwa ujumla. 
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: