Professa J akiwa na Afande Sele Morogoro.

 Professa J amesafiri hadi mkoani Morogoro kwenda kuhudhuria mazishi ya aliyekuwa mke wa msanii mwenzake Afande Sele.

Kupitia Instagram, Professa J ameshare picha akiwa kwenye mazishi na kuandika: Msibani Morogoro nyumbani kwao marehemu Asha au mama Tunda sasa hivi… tunajiandaa kwenda kumpumzisha kwenye nyumba yake ya milele saa kumi jioni ya leo, bwana alitoa bwana ametwaa, jina la bwana lihimidiwe…. Amen
Jeneza la marehemu likiwa nje pamoja na watu mbalimbali waliojitokeza katika mazishi hayo.

Awali Afande Sele alisema kifo cha Mama Tunda kimetokana na uzembe wa madaktari. Mama Tunda alifariki baada ya kulazwa kutokana na kuugua Malaria. Akizungumza na Bongo5 leo, Afande alidai kuwa bila uzembe wa madaktari huenda malaria isingechukua uhai wa Mama Tunda.

Afande Sele akilia kwa uchungu.

“Mama Tunda ametuachia pengo kubwa sana kwenye familia,” alisema Afande. “Amefariki jana saa tano usiku katika hospitali kubwa hapa Morogoro kutokana na uzembe wa madaktari. Walimpa matibabu akarudi nyumbani, sitaki kulizungumzia kiundani kwa sasa hivi kwa sababu tupo kwenye wakati mgumu.
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: