DSC_0741
Mgeni rasmi Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Iringa Dkt. Leticia Warioba ambaye pia ni Mkuu wa Wilaya ya Iringa akizindua rasmi kampeni ya SHUGA Redio ambapo amewaasa Vijana kuzingatia matumizi sahihi ya Kondomu na upimaji wa VVU ili kuzitambua afya zao mapema na kuepukana na maambukizi mapya ya VVU.
DSC_0757
Mkuu wa kitengo cha watoto na Ukimwi kutoka UNICEF, Alison Jenkins akizungumza kwenye uzinduzi huo ambapo amesema Lengo kuu la kampeni ni kusaidia juhudi za serikali katika kupunguza maambukizi mapya ya VVU miongoni mwa vijana wa umri wa kubalehe kupitia vyombo vya habari na kuwafikia kwa ujumbe mahususi kuhusu upimaji wa hiari na ushauri nasaha na ngono salama. Kampeni inakusudiwa kuchochea vijana walioko kwenye hatari kubwa ya kupata maambukizi waweze kutafuta na kuziendea huduma zilizopo.

Bi. Jenkins aliongeza kuwa kutakuwa na mfululizo wa vipindi 12 vya kuigiza wenye muda wa dakika nane umeelezea maisha ya vijana wanne (Sofia, Fally, Amina na Kavis) kuwakilisha vijana wa umri wa miaka 15 – 24. Simulizi iliyopo inahusu ndoto, chaguzi, marafiki, mapambano ya changamoto za kimaisha katika Dunia, ambayo UKIMWI ni tishio kubwa.Simulizi hizi kwa ujumla wake zinajikita kwenye somo la mbinu za upimaji wa VVU na ushauri nasaha, matumizi ya kondomu katika mahusiano ya muda mrefu , Kinga, unyanyasaji wa kijinsia na kingono, unywaji pombe na athari za kuwa na wapenzi wengi zinazopelekea kupata maambukizi ya UKIMWI.
DSC_0765
Mgeni rasmi Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Iringa Dkt. Leticia Warioba ambaye pia ni Mkuu wa Wilaya ya Iringa akimpongeza Mkuu wa kitengo cha watoto na Ukimwi kutoka UNICEF, Alison Jenkins (kulia) kwa risala nzuri wakati wa uzinduzi huo. Kushoto ni Kamishna wa TACAIDS na Balozi wa Vijana (UNICEF) na Kampeni ya SHUGA Redio, Faraja K. Nyalandu.
DSC_0694
Mratibu wa TACAIDS Mkoa wa Iringa, Bw. Owen Wimbo miongoni mwa wadhamini wa kampeni hiyo akizungumza machache na wakazi wa Iringa, Vijana na wageni waalikwa waliohudhuria sherehe ya uzinduzi wa kampeni ya SHUGA Redio iliyozinduliwa rasmi jana kwenye viwanja vya Samora mkoani Iringa.
DSC_0706
Kamishna wa TACAIDS na Balozi wa Vijana (UNICEF) na Kampeni ya SHUGA Redio, Faraja K. Nyalandu, akizungumza na vijana waliohudhuria uzinduzi huo ambapo aliwaasa kutouza mechi kusubiri muda muafaka na kuzingatia zaidi masomo sanjari na kuepuka kufanya ngono zembe.
DSC_0770
Mgeni rasmi akiwa ameungana na wasanii wa Bongo Flava pamoja na meza kuu kwa ajili ya kuzindua rasmi kampeni ya SHUGA Redio.
DSC_0774
Sasa imezinduliwa rasmi.....!
DSC_0653
Msanii wa muziki wa Bongo Fleva nchini Ben Paul akitoa burudani ya aina yake iliyoambatana na ujumbe mahususi wa kuhamasisha vijana kupima afya zao wakati wa uzinduzi wa kampeni ya SHUGA Redio ulioanyika jana mkoani Iringa kwenye viwanja vya Samora.
DSC_0931
DSC_0679
Umati wa vijana na wanafunzi wa shule mbalimbali za sekondari Iringa wakishuhudia burudani za wasanii maarufu wa Bongo Flava waliosinfdikiza uzinduzi huo.
DSC_0685
DSC_0793
Pichani juu na chini ni msanii wa muziki wa Hip Hop nchini anayejulikana kama Izo Business akitoa burudani kwa Vijana na wageni mbalimbali waliohudhuria uzinduzi wa Kampeni ya SHUGA Redio iliyozinduliwa rasmi jana mkoani Iringa kwenye viwanja vya Samora.
DSC_0815
DSC_0268
Baadhi ya wanafunzi wa Kituo cha Upendo mjini Iringa wakiwa kwenye foleni ya kuingia kwenye chumba maalum kwa ajili kupima Virusi vya Ukimwi bure wakati wa sherehe za uzinduzi wa Mradi wa SHUGA Radio uliofanyika kwenye viwanja vya Samora mjini Iringa.
DSC_0274
Mtaalamu kutoka AMREF akichukua vipimo vya damu kutoka kwa mmoja wa wanafunzi wa kituo cha Upendo mjini Iringa aliyejitolea kupima kwa hiari Virusi vya Ukimwi wakati wa uzinduzi wa Mradi wa SHUGA Redio unaotekelezwa kwa ushirikiano wa Mashirika ya Kimataifa moja linaloshughulikia Huduma za Watoto (UNICEF), Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO) sambamba na Redio Jamii 10 nchini Tanzania wenye lengo la kuendeleza kampeni za hamasa kwa vijana kupunguza maambukizi mapya ya VVU.
DSC_0175
Vijana wa kiume nao walihamasika kupima afya zao bure bila malipo.
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: