Mwenyekiti wa Taifa Taso, Engelbert Moyo akifafanua jambo wakati wa mkutano na waandishi wa habari leo.
Ofisa Mtendaji Mkuu wa EAG Group, Imani Kajula akifafanua jambo wakati wa mkutano na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam, kuhusu ushirikiano wa kampuni hiyo na Umoja wa Wakulima Tanzania (TASO), katika kuhamasisha kilimo na maonyesho ya Nanenae yatakayoanza Agostii 1-8. Kulia ni  Mkuu wa Biashara EAG Group, Mathew Gugai na Mwenyekiti wa Taifa Taso, Engelbert Moyo.
 Baadhi ya waandishi wa habari wakiwa katika mkutano huo.

Na Hellen Kwavava wa Kajunason Blog.

Rais wa mapinduzi ya Zanzibar Dkt Ali Mohamed Shein anatarajiwa kuwa mgeni rasmi katika maonyesho ya kitaifa ya nane nane yayotarajiwa kufanyika mkoani Lindi.

Dhumuni la maonyesho hayo kwa kila mwaka ni kutoa msukumo maalum nchini katika kuinua kiwango cha kilimo, ufugaji pamoja na kuhimiza hifadhi ya mazingira.

Akizungumza na waandishi wa habari leo jijini Dar es salaam mwenyekiti wa wandaaji wa maonyesho hayo (TASO) Engelbert Moyo amesema kwamba maonyesho hayo ya kilimo yana lengo la kutoa mafunzo pamoja na elimu ya kilimo na ufugaji bora kwa wakulima na wafugaji wote.

Aidha mwenyekiti huyo ameeleza kwamba chama chao kinazingatia kukuza na kuendeleza kilimo, mifugo pamoja na uzalishaji wa bidhaa za maliasili.

Naye Afisa mtendaji mkuu wa kampuni ya EAC Group Limited Imani Kajula amesema kwamba inatakiwa kuchukulia kilimo kama niajira iliyo rasmi nasi vile watu wanavyo kichukulia.

Mbali na maonyesho hayo kufanyika kitaifa Mkoa wa Lindi ila katika kila kanda yataendelea kufanyika ambapo mikoa ya Arusha, Mbeya, Dodoma, Morogoro, Tabora pamo jana Mwanza.
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: