Barabara ya Songea-Namtumbo yenye urefu wa Kilometa 71.4 kama inavyooneka na katika picha
 Waziri wa Ujenzi Dkt. John Pombe Magufuli (Mb) akisalimia niana viongozi wadini kabla ya ufunguzi rasmi wa Barabara ya Songea –Namtumbo yenye urefu wa Kilometa 71.4 katika Wilaya ya Namtumbo mkoani Ruvuma.
Waziri wa Ujenzi Dkt. John Pombe Magufuli (Mb) wa kwanza kushoto akimtambulisha Mbunge wa Namtumbo Ndugu Vita Kawawa kwa Mwakilishi wa Serikali ya Marekani na kutoka kwenye Mfuko wa Changamoto za Millenia MCC Karl Freicker katikati. Kulia ni mwakilishi kutoka Benki ya Maendeleo ya Afrika Bi. Tonia Kandiero.
Baadhi ya watendaji mbalimbali wa Taa sisi na Wenyeviti wa Bodi zilizopo chini ya Wizara ya Ujenzi wakimsubiri Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Jakaya Kikwete katika sherehe za ufunguzi wa barabara ya Songea - Namtumbo na Uwekaji wa jiwe la msingi barabara ya Namtumbo –Matemanga katika Wilayaya Namtumbo Mkoani Ruvuma.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi Mhandisi Mussa Iyombe kulia akipokea cheti kutoka kwa Katibu Mkuu wa wizara ya Fedha, Dk. Servacius Likweli leka maishara ya makabidhiano ya barabara ya Songea - Namtumbo kutoka kwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Jakaya Kikwete akimshukuru Mwakilishi wa Serekali ya Watuwa Marekani Ndugu Karl Freicker mara baada ya Rais kuifungua Barabara hiyo ya Songea - Namtumbo.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Jakaya Kikwete akiweka jiwe na Msingi barabara ya Namtumbo - Kilimasera - Matemanga 128.9km huku akishuhudi wana Balozi mdogo wa Japan, Mwakilishi kutoka Benki ya Maendeleo ya Afrika (ADB) pamoja na Waziri wa Ujenzi Dkt. John Pombe Magufuli.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Jakaya Kikwete akikata utepe pamoja na viongozi mbalimbali kutoka Serikali ya Marekani, Wabunge, Mawaziri na viongozi wengine kuashiria ufunguzi rasmi wa barabara ya Songea - Namtumbo 71.4km - Picha zote na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini, Wizara ya Ujenzi (GCU).
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: