Na Mnyetishaji Wetu, Mitandao ya Jamii.

Kauli ya Ommy Dimpoz aliyoitoa siku mbili zilizopita akishauri wadau wajitokeze na kuwekeza zaidi katika kununua vifaa vya kisasa ili wasanii wasipate sababu ya kwenda kushoot video zao nje, imewafanya madirector nao kutoa yao ya moyoni.

Kauli ya Ommy Dimpoz imetokana na maswali ambayo watu wengi wamekuwa wakihoji kwanini wasanii wengi sasa hivi wanaamua kwenda kushoot video zao nje na kwa gharama kubwa ili hali inaaminika hapa nyumbani bado kuna maeneo mengi na mazuri ya kufanyia video ambayo hayajatumika.

Baada ya Nisher kuzungumza na kuwatupia lawama wasanii kuwa wanawadharau madirector wa Tanzania, Adam Juma wa Visual Lab na yeye ametoa ya moyoni kuhusu kauli hiyo ya Dimpoz, kupitia Instagram ameandika:

“Hahahahahahha vifaaa tutanunua inshallah, ila sasa nasisi tutaanza kutangaza bei mnazotulipa! Sijawahi kulipwa zaidi ya mil 3.5 na msanii yoyote Tanzania kama yupo aje nitampa video 10 buree. @rehemavisuallab @nisherbybee @jerrymushalastudios @hefemi @meckykaloka # niggarstalkingshit#mnanitibuasasa#noneducatedniggasoncrack#.”

Director Jerry Mushalla na yeye alicomment kwenye post ya Adam:
“Most Musicians like to blog and talk too much... But when it comes to actual payments they don’t pay… @adamjumanxl I wish directors woote mngekuwa na msimamo wa pamoja @hefemi @nisherbybee @abas_adam @travellah”.

Na hiki ndicho Nisher alichokisema wiki hii kuhusu swala hilo:
“Mi sipati logic wasanii wanavyosema wanaweza kulipa sijui milioni za hela wapi… mimi napigiwa simu na wasanii wakubwa lakini kila anayekupigia anasema mimi sina hela lakini, naweza kukugharamia chochote unachotaka tushoot video.

Unaanzaje na kauli halafu na wakati mimi nasoma kwenye internet kwamba umelipa sijui kiasi gani gani gani kwenye video fulani fulani, nafikiri video ya Ben Pol juzi tu ambayo tuliifanya ‘Unanichora’ labda ndiyo video niliyopata hela nyingi kwa kiasi fulani kwa sababu video iligharimu karibu milioni 10 hivi. Mimi nadhani tunachukuliana poa.

Kwa Mfano ukinilipa milioni 5 au 10, una uhakika kwamba hela hiyo hiyo itatumika kusambaza kazi yako […] kufanya kila kitu. Vyombo vipo cranes nini, cranes zenyewe za kukodi kwa siku laki 5, camera zipo za kukodi Red Camera unaambiwa labda dola 800 kwa siku, nani atakupa hiyo hela? Hivi vitu vinakatisha tamaa wasanii hawatukubali wanatuona kama hatujui.”

Hiki ndicho alichokisema Ommy Dimpoz wiki hii na kuwafanya madirector nao kuamua kufunguka:


“Biashara ya video ishaingia ushindani, kwahiyo kuna haja ya kuwekeza kwenye vifaa, mimi na uhakika hapa mtu ana mavifaa kibao unaenda kushoot Lushoto huko noma, wazungu wenyewe watauliza umeshoot wapi. Tuna maeneo kibao Zanzibar wapi wapi wapi ya kufanyia video, sio kwamba hatuna maeneo, maeneo tunayo lakini hatujawa na vile vitu. Kwahiyo ndiyo maana hata mtu pia unafikiria aha! sijui nishoot Zanzibar, lakini unawaza kumchukua labda GodFather au nani kumleta huku Tanzania ndiyo mziki.


Halafu mtu utakapoleta vifaa hivyo na uhakika hautaishia kwenye video tu, kuna matangazo, utakodi utafanyaje… Watu lazima waelewe kitu kimoja kwamba hakuna mtu anayependa kujitia gharama kama kuna uwezo wa kuepuka gharama, sio ufahari mimi nina vitu vingi vya kufanya sio kwamba nataka tu nikalipe dola elfu 30 kushoot video wakati nina uwezo wa kuokoa hiyo hela labda kulipa dola elfu 15 au elfu 10.

Wadau wanatusikia sie ndio wasanii wenyewe tunasema kwamba muziki unalipa mnaona sasa hivi vijana wenu wanapata shilingi mbili tatu, hizo shilingi mbili tatu mtagawana nao vipi kuliko kwenda kuwapa watu wengine huko nje ya nchi.
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: