Mbunge wa Bumbuli na Naibu Waziri wa Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia.
January Makamba.

Katika pita pita yangu ndani ya mtandao wa Jamii (Facebook) nilikutana na maneno ya January Makamba akikazia kauli yake ya kuonyesha nia ya Kugombea Urais 2015. Aliyasema haya;

"Uongozi wa kizazi kipya upo tayari kushika hatamu za uongozi na kuijenga Tanzania mpya, kwa fikra mpya na maarifa mapya. Mabadiliko, kokote yalikotokea, yalidaiwa na kuongozwa na vijana. Vijana wa Tanzania washike usukani wa kuleta mabadiliko wanayoyataka. Ukiona kijana anamwambia kijana mwenzake hana uzoefu, basi kazi ya kuleta mabadiliko ni kubwa zaidi. Kutokuwa na uzoefu ni sifa ya kijana. Tusi kubwa kwa Obama mwaka 2008 lilikuwa ni kukosa uzoefu, kukosa rekodi. Tusi hilo lilikuwa muziki kwa wapiga kura wa Marekani. Tanzania mpya inahitaji viongozi wapya, mazoea mapya, fikra mpya na maarifa mapya. Inahitaji kuthubutu mambo makubwa sio kulinda uzoefu wa nyuma". Tunaweza.

Jackson Kalikumtima: Now I have two Candidates for Presidency 2015.
1. Edward Ngoyai Lowasa - tested with good follow up and implementation records

2. January Makamba: - young, energertic and full of new ideas to take Tanzania to the next level.
Sitajali wakinipa yeyote kati ya hawa wawili.

Joseph Shaluwa: Hao vijana tutawaweka kuanzia huku chini kabisa. Tuwachague wenyeviti wa serikali za mitaa vijana, madiwani, wabunge vijana ambao watawazaa mawaziri vijana kisha rais wetu ajaye pia tunataka awe kijana mwenye nguvu. Mtazamo mpya na matumaini mapya. Inawezekana!

Jerry Kagose: Ni kweli kwa sasa Tanzania, tunahitaji mtu wa kweli, na kijana makini, Tanzania sio masikini ila tumekosa viongozi makini, our country it's has been poorly managed.

Joseph Shaluwa: Nakubaliana na wewe January.

Elihud Sekumbo Junior: My brother i bilieve hata tukikupa nchi bado utaingia na baraza bovu la mawaziri huna vijana smart wanaoweza kufanya siasa safi Vijana wote wa Ccm waliopo wanaweza siasa za mipasho, matusi na kukatili laiti ungekuwa na wasindikiza wazuri tungekupa nchi

Lusekelo Andrew: Sio kweli kabisa kua fikra mpya na maarifa mapya zinaweza kuletwa na vijana pekee. hakuna mausiano chanya ya moja kwa moja kati ya Uongozi na Ujana hakuna! rika kamwe haijawahi kua sifa ya Uongozi bora, tusiweke mifano kadhaa kurasimisha hoja ya Rika kua Sifa kuu ya Uongozi. hebu tuwekeze katika sifa za kiongozi bora, then watu watapima tuu..wala haihitaji kutumia muda mwingi kushawishi katika baseline ya Ujana. Tanzania we need Leaders, not Age. vijana tusiingie kwenye mtego wa kutamani kuongozwa na Umri/Rika, tutazame wapi tunataka kama Taifa kufikia then nani tunadhani ni kiongozi kweli wa kusaidia Taifa likafika huko tunakotaka. maneno ya wanasiasa hayajaanza leo, yalikuepo na yapo mpaka hapa tumefika! we need TRUE Leaders, Leaders with greet Commitment, +ve desire, Convictions and great Visions for our Nation. Leadership has never be defined in terms of AGE!, never!! but Potential and Leadership Qualities. hoja ya umri kamwe isitutoe kwenye Focus ya wapi tunataka kufika kama Taifa, na wakutufikisha huko kamwe SIO Kijana bali ni KIONGOZI. Vijana tusijiweke wepesi kupita kiasi. this is our Nation, hakuna wa kutusaidia kufikiri kwajili ya Taifa letu.

Zion Man Seme: makamba porojo siyo nzuri,Tunahitaji kiongoz atakaye sema trafik rushwa basi na jeshi zima la police kuheshimu haki za rai,Rais atakaye leta mabadiliko ktk Elimu ambayo itamsaidia ktk mazingira yake badala ya hii kumuanda mtu kuajiliwa pia na maslahi bora kwa mwalimu na mazingira ya kazi bora,Tunahitaji Rais atakaye simamia rasimali za taifa na kufaidika nazo na maisha yawe bora kwa kila mtanzania,Hosptali kuanzia ngazi ya taifa hadi kijijini ili vifo vya akina mama na watoto viishe,Barabara bora kila sehemu ya nchi,kilimo kilicho na tija kwa mkulima,maji safi na salama na miundo mbinu mizuri,Kuliondoa Taifa ktk kutegemea kutoka kwa hisani bajeti yetu ili taifa liwe huru kiuchumi,kisiasa,kiutamaduni na kifikra,Tunahitaji Rais atakaye kwenda kinyume na sera za kimaghalibi kisiasa awe mzalendo,Rais atakaye simamia uadilifu na uaaminifu wa Raia na watumishi wa umaaa ngazi zote taifa hadi kijiji nakurudisha heshima ya Taifa na uzalendo,Tunataka Rais mwenye maamuzi magumu wakati wote Taifa linapoangamia kisiasa kiuchumi,kiutamadumi na kifikra Atatufaa sn .Km unawito huo makamba Anzisha safari ila km hauna bro potezea tu hiyo nafasi maana hukumu yke majeraha yke afadhali ufe.Hutaki porojo za siasa ambazo zina maslahi ya vyama vyenu na familia zenu kamwe hutashinda ukiwa na dhamira tofauti na hizo.

Daniel Simon Mwakimi: Hata JK alikuja na gia ya ujana lakini mpaka anazekea ikuru amefanikiwa kuongeza deni la taifa tu, kijana nisie na imani na vijana.

William Sunday Sempoli: Tatizo sio umri wa mtu, unaweza ukawa kijana mwenye mawazo ya kizee na unaweza ukawa mzee mwenye mawazo ya ujana! Tanzania tunamhitaji mtu mwenye uwezo wa kututoa hapa tulipokwama na kutupeleka mbele! Nchi hii ni kama gari lililokwama kwenye matope,tunahtaji tingatinga la kututoa ktk matope haya. All in all Big Up bro kwa kuthubutu kutangaza nia ingawaje chama kilikua kimewapga stop! ila Kinana alishakusafisha akasema huna kosa!

Cleophas Cyprian: Kabla ya kuchagua vijana mwaka 2015,ninyi mliopo sasa ilitakiwa muoneshe uwezo wenu katika kulipigania taifa kwa matendo na sio maneno,ww kama waziri kijana umefanya nini kwa kipindi hiki katika kulitetea na kulipigania taifa ili liondokane na maadui wa umaskini,maradhi na elimu,au umeendelea kutetea mfumo wa chama kwanza taifa baadae:Katika viongozi vijana tulionao sasa ni Deo Filikunjombe ndio ameonesha uwezo katika kulipigania taifa na si vijana wengine ambao wamekuwa wakitetea maslahi ya vyama vyao tu.

Shard Cole: Hizo kick za ujana peleka bumbuli, kwani zishapitwa na wakati, Baba yako JK naye alikuja na gia hiyo hiyo ya ujana lakini leo tunajuta, so we as Tanzanians we can not repeat same mistake coz its a sin.

Emil Lukiko: Tatizo sio wewe Mheshimiwa, tatizo ni chama chako.

Boniphace Maganga: Mnataka urais kwa kigezo cha ujana?
1.Kwa nini mikataba ya madini mibovu hampigi kelele?
2. Kwa nn mikataba ya gesi inautata hamhoji?
3.kwa nini vijana hawana ajira wamejaa mitaani hamjaja na mjadala mpana kama vijana kuwasaidia vijana wenzenu?
4. kwa nn mko kimya rasilimali za nchi zinaondoka?
5. kwa nn mpo kimya na nyie vijana maadili ya taifa yanapolomoka?
6. Kwa nn mko kimya demokrasia yetu haiko huru?
7.kwa nn mko kimya wakati watoto wanabakwa,tembo wanauwawa?
8. Kwa nn mko kimya uchumi wa nchi haukuwi?
9. kwa nini mko kimya elimu yetu haieleweki?
10. kwa nn mko kimya bungeni vijana bila kuwa na mjadala mpana wa kitaifa kama vijana wabuge kwa masuala ya kitaifa?
Vijana mmepewa nafasi nyingi na mh. Rais kikwete mpo bungeni vijana wengi mbona hamsimami kama vijana na kuweka pembeni maslahi ya vyama vyenu? Nini mnafanya kusaidia vijana na taifa? Kuna vijana wengi mno ma dc wanafanya nn? Hii ndio hofu yangu kwa vijana wezangu wa karne hii mmejaa ubinafsi sanaaaaaaaaaaa wala humna mawazo mapya ila uloho wa madalaka. Ngoja tusibiri.

Method Nyakunga: Tatizo cyo tu kizazi kipya! je mifumo nayo ni mipya? Kama mifumo ni hii iliyopo basi labda kizazi kipya kitokane na vyama vya upinzan kwani ndani ya chama tawala kwa namna kilivyo sasa kimehodhiwa na wa2 wachafu wa kila aina wanaoangalia masilah yao2 hivyo hata atokee m2 ndani ya chama tawala itakuwa ngumu sana kutekeleza mambo ya maendeleo kwani hawa wadhalimu kama wataona maslah yao yanaguswa hakika watamkwamisha2 kama tunavyoona sasa hivi wamekwamishi sheria nyingi2 zenye maslah kwa taifa kama vile sheria za mapato,sheria za uhuru wa habari,sheria za makosa jinai, sheria za uadilifu kama hv juzi baadhi ya wabunge wa chama chako walipendekeza uwajibikaji na uadilifu visiwe tunu za taifa sasa bro cjui umejipangaje ila naamini hakuna kinachoshindika chini ya jua niko nyuma yako ila utafakari mara3 ni kwanini tumefika hapa? Mungu akubariki kwa uthubutu wako na akuonyeshe njia #Amina

Mzalendo Joseph Goliama: Uko sawa kwa upande mmoja lakini kwa upande mwingine kauli hizo ni za ubaguzi wa rika, nchi yetu na katiba ya nchi yetu inataka Rais atokane na watanzania wenyewe ,mtanzania mwenye uwezo na mwenye sifa ,mzalendo, mtu wa amani wa upendo na wa haki bila kujali jinsia yake na Rika lake ndiye anayestahili kuchukua uongozi wa Taifa letu, kauli za kibaguzi kama hizo ni uoga , kuogopa kuingia kwenye kinyang'anyilo na watu wazima mnaowaita wazeee sisi vijana wazalendo tunaona sio haki, kama mmeamua kugombania nafasi hiyo lazima mjiamini lazima mkubali kushindana na watanzania wa jinsia zote bila kujali Rika.......mimi naamini kijana mwenye sifa, mwenye uwezo, mwenye uzalendo hawezi akatoa kauli zakuwatoa wengine ulingoni kwani sifa na uwezo wake ndio ngao zake.

Sadam Ibrahim: Hata mwenye uzoefu alianza bila uzoefu, kuthubutu ni suala la msingi... pamoja sana kiongozi.

Hildegarda Kiwasila: Nani atawaweza watanzania ambao hupenda easy come easy go. Akipata mkopo wa kusoma suala si kukazana na masomo-ni kununua gari, mitumba mwenge, kushinda bar mpaka allowance iishe. Darasani ni vivalo na kushindana magari. Mpangie vijijini-hakubali anarudi mjini. Mtengenezee barabara na mifereji ya maji ya mvua-anajaza maroba na masanduku ya solid waste na kuunganisha choo hataki kuchangia uzoaji taka anatupa malundo usiku barabarani. Anavamia ardhi erti hailimwi miaka na huyo mmiliki-anaiuza yeye halimi. Ni kuvamia, kujigawia, kuuza. Uzoefu wa kazi unaupata kazini kama unania ya kutumia elimu uliyopata, democratic decision making na dialogue na uliowakuta na kusikiliza ushauri mzuri na kuuchunguza kutoka wengine. Kusikiliza maoni ya walengwa na watoa huduma. Mla rusha ni ndugu yetu, jirani au rafiki. kama ndugu wamjuao wanamlinda-serikali itawezaje kumjua bila ya umoja wetu. Hakuna chama kisicho na upendeleo-kama si udugu na ukabila ni udini na urafiki. Umefika wakati kila mmojawetu awajibike na utendaji wenye ufanisi, uwazi na ukweli, kujituma ni muhimu kwetu wote. Mtu yupo kijijini au nje ya mji hata kulima wala kakaa tu. Matumizi ya raslimali yasiyoi endelevu, matajiri wasioungana na kufanya kweli. Wakandarasi vibaka hawatimizi ujenzi utakiwao, bangi, madawa ya kulevya na kuuza m,itumba na vipodozi ndio miradi ya kutusaidia kujikwamua au kuongeza magonjwa ya figo na vilema kwa watoto. Kuzurura kilometa 10+ kutwa kutembeza wanja na chupi za mitumba kijana kifua cha miraba mine hakutotifikisha mbali. Tukubali kupambana kimaendeleo ingawaje ukweli unauma lawama ndio tija kwetu.

Clarin Wilson: Yangu mawili tu ndg. Makamba.
1. Sina hakika kama unamuda wa kusoma maoni ya wachangiaji.
2. Naunga mkono hoja kwasababu zifuatazo
A. Nchi ilipopata uhuru iliongozwa na vijana enzi ile mwalimu na wasaidizi wake walikuwa vijana na waliweza kuongoza kwa hali ya wakati ule.
B. Fikra ya busara kuwa ipo kwa wazee tu sio kweli Mungu..wapo vijana ambao Mungu amewaanda kuwa lango la kupitisha baraka kwa taifa na mataifa.
C. Tetesi za kuwa mh.JK alizuiwakugombea mwaka 1995... zilipoteza haki ya vijana kujiamini kuwa wanaiweza nafasi ya uraisi.
D. Kule umasaini kuna kundi la Morani hawa ni vijana askari ambao ulinda na kuhakikisha maendeleo ya jamii yao yanasonga mbele..ukitoka hapo unaingia kwa Oraiboni wazee kazi yao kubwa ni kutoa ushauri tu kwa hao Morani.sababu kubwa walishapitia ktk nafasi ya umorani.so vijana tunaweza
E. We nishahid angalia kwenye sekta binafsi hapa Tanzania mfn..mtandao. .mabenki ..mahotel...na kampuni tofauti za uwekezaji wanaofanya kazi ni vijana wasomi na hakika wanaleta mafanikio...
F. Ni fikiria kwann Majaji wa mahakama kuu wamepewa wasaidizi..maarufu kama makatibu wa majaji...kundi kubwa la hao wasaidizi ni vijana smart husaidia kuandika hukumu na mambo mengine mengi.

Mwisho nakupongeza kwa kutangaza nia yako...lkn sina uhakika kama umefanya jambo la busara kutangaza nia mapema hvyoo...tayari najua chama chako kinajua nijinsi gani ulivyo jembe na fitina zimejaa hapo...unanipa wasiwasi wa kukosa kukuita Raisi awamu ijayo..hao wazee wanafitina kubwa snaa...ulipaswa kuwaonesha iyo ndoto yk nasio kuwaambia...zaidi nakutakia mbio njema.

Anthony Mtaka: JANUARY MAKAMBA - BINAFSI NIMEKUWA NIKIKUAMINI WEWE KAMA MOJA YA VIONGOZI NA MTU MWENYE UWEZO MKUBWA WA KUPAMBANUA MAMBO, SIJAWAHI KUFANYA HIVYO SABABU YA UMRI WAKO WA UJANA, UONGOZI SII MZIGO WA ZEGE WALA GUNIA LA MKAA KWAMBA UKIWA MTU MZIMA UTAKUANGUSHA NA WALA UONGOZI SII MBIO ZA KUFUKUZA UPEPO KWAMBA UKIWA KIJANA BASI UTASHINDA, WAMAREKANI ULIKOSOMA WEWE HAWAKUMUUNGA MKONO OBAMA SABABU YA HAIBA YAKE YA UJANA, BALI WALIAMINI KWAMBA CHANGAMOTO ZAO OBAMA NI MTU SAHIHI WA KUZITATUA KWA NAMNA YA UJENGAJI WAKE WA HOJA, UTAYARI WA MOYO WAKE KUJITOA KWA AJILI YA WENGINE, NA SIFA ZINGINE ZAIDI NA ZAIDI, VIJANA WA TANZANIA HAWAITAJI KIJANA WA KUTATUA SHIDA ZAO,BALI WANAHITAJI MTU ANAYEGUSWA NA HOJA ZAO, SIKU ZOTE TUMEKUSHAHABIKIA WEWE JANUARY MAKAMBA SII SABABU YA KUWA WAZIRI MDOGO AU MSAIDIZI WA MH. RAIS UKIWA NA UMRI MDOGO, BALI TUNAAMINI NI MOJA YA BINADAMU WENYE WELEDI WA MAMBO, MUNGU AMEKUJALIA UWEZO NA HEKIMA, TUNAO VIJANA WENZAKO WENGI WA HOVYO NA WANA DHAMANA, KAMA TULIVYO NA WAZEE WENGI AMA WENYE HEKIMA AU HOVYO PIA, NAJUA UNA UPANA WA MAMBO MENGI, SITAKI KUAMINI KAMA UWEZO WA KIUONGOZI, HEKIMA, BUSARA, UZALENDO NA AINA NYINGINE YA SIFA ZA KIONGOZI VINA UHUSIANO NA UMRI, MIMI SII MUUMINI WA DHANA YA UZOEFU KATIKA PERFORMANCE YA MAJUKUMU, NA PIA SII MUUMINI WA DHANA YA UMRI KATIKA UTEKELEZAJI WA MAJUKUMU, DUNIA IMEPATA MABADILIKO SII KWA SABABU YA VUGUVUGU LA UMRI WA VIJANA, BALI KWA SABABU YA WATU WALIOJITAMBUA NA WENYE UTHABITI WA UZALENDO KATIKA KUPIGANIA HAKI NA MASLAHI YA WENZAO WENGI,KAZA BUTI, MIMI NAUNGA MKONO NIA YAKO LAKINI SIFANYI HIVYO SABABU YA UJANA WAKO.

Adriano Mawazo: Namuunga mkono Jenifer tatizo si kijana bali ni mfumo wa chama chako kilivyo. Hata ukiwa wewe lazma utafuata matakwa ya wachache ya chama chako hutaweza kuwasaliti vibabu vya chama chako ambao tangu nipate akili bado vipo ndani ya chama unategemea kutakua na mabadiliko wakati umeapa kufuata katiba ya chama chako.tusidanganyane sera za chama chenu ni mbovu na nizakikandamizaji.miaka ijayo watoto wa vigogo weng mtajazana bungeni.sasa usawa upo wapi.wapitishao majina ya wagombeao ni hao hao baba zenu na mama zenu ndani ya chama.sasa mkiongoza mtawasaliti waliowachagua?tusidanganyane tunahitaji mabadiliko ya kweli c huu uchaf wa kindugu wa chama chenu.

Mikhail Frank: Tuache Sound jamani,tunataka kiongozi bora sio ujana au uzee,vijana wangapi wako bungeni ni wachache sana waliothubutu wengine chenga tupu,Hoja ya Ujana me napinga kabisa,aisee kwa nchi ilipofikia sasa inahitaji kiongozi anaejielewa kweli na mwenye dhamira ya dhati ya kututoa tulipo,hapa,jamani Ikulu sio kijiwe cha kwenda kufanya Internship pale.nimemaliza.

Allen Crony Kasamala: Hongera mheshimiwa kwanza kwa hatua hiyo ya maamuzi, lakini ushauri wangu ni kwamba lazima twende mbali zaidi ya platform ya ujana na au uzee, kuna masuala mengi ya msingi yanayolikabili Taifa hili kubwa zaidi ni RUSHWA, kubebana, kumomonyoka kwa maadili, kulindana, kutokutii sheria na taratibu zilizopo, commercialization of education, kushuka kwa kiwango cha uzalendo za mapenzi kwa Taifa, kupoteza imani kwa vyombo vya umma kama polisi, mahakama,taasisi, wizara nk, tunataka uongozi wenye uwezo wa kutizama nyuma na kusema TULIKOSEA hapa, sasa tuparekebishe na kusonga mbele bila kupepesa macho, we need a neutral leadership na SI uongozi wa kulipa fadhila at our expense, its my prayer that the debate will go beyond the cheap rhetorics of ujana na uzee, history has recorded vijana waliofanya vizuri na waliofanya vibaya pia hivyo hivyo kwa wazee, hoja hiyo haiwezi kuwa ndio defining criteria, personally i have nothing against you and your aspirations, in most i want the horizon to be expanded further, hata kama hii ni 'strategy' basi tusisahau pia kwamba wazee pia si wa kupuuzwa, tusiwahukumu kwa kuwa tu ni wazee, mimi ni kijana, but i want to see this from a neutral and sober eye, otherwise May God lead your way.

Finehas Daud Mwihambi: Makamba umenena kwa nafsi yako 'watz wanamajeraha mengi yaliotokana chama twawala jk aliposhika dola kwa kigezo cha ujana -tulipata matumain ya maisha bora lkn maisha yakawa balaa neema ikawa kwa wanasiasa .mzee Makamba akateuliwa katb wake ndo ikawa balaa zikaanza siasa za kibabe matumain yakapotea unaweza kuthubutu .lakin utakuwa kama remote kwa kulinda maslai ya chama chako na mabepar wake.

Elihud Elias: Kaka umejaliwa porojo nzuri ka mzee wako ila najua unatak uendeleze ufalme wa mzee makamba ktk nchi..so kick nzuri umeona ni ujana POLE tumekushtukia sisi tunataka VIONGOZI BORA ambao wataivusha tz yetu mbali.mimi ni kijana mpaka hapa kura yangu iwe ni ww au kijana yyte from ccm ashaikosa sababu ccm yenu ni ya ulaji imekosa ufanisi mzuri wa kuyekeleza sera zenu nzuri mlizoishia kuziandika ktk vitabu vyenu...toeni ufisad na urasimu kwenye chama chenu then njooni kwetu wananchi.

Godfrey Madegwa: Mimi najua umekuja tu kujaribu kwa tiketi ya ujana ili ikifikia muda useme sasa niko tayari...unataka ujiandae baadae bila ya kuandaliwa...unataka uje na staili ya "hazikutosha"kama Kikwete 95 ili urudi 2025....hahahaha umetutega...!!?? ila wa TZ wa sasa sio waleee wa 95 na wa leo sio wa 2025 tutakua balaa kifikra....bado bumbuli wanakuhitaji na huko unaweza....mfumo wa viongoz vijana bado katik nchi changa...mfumo wa kiongoz mwanamke bado katk nchi kam Tanzania hata huyo mwanamke awe Prof wa uchumi...hatujaaminishwa hivyo...Rais kikwete aliwah sema zipo sehem haki sawa lakin huwez mchagua Mkuu wa majeshi Mwanamke...hata IGP au CGP huwezi...!! sembuse Rais...?! ujana upo lakin bado kuna sehem tunapwaya....ila uko vzr bt kwahili am sory.

Athuman Makange: Hizo gia zaujana peleka bumbuli hatuhitaji kijana kutuongoza tunahitaji kiongozi mwenye kuona changamoto za nchi kwamapana yake nakuwa na uwezo wakuzitatua nasi ujana kama kofia yakumpa uongzi nakuendeleza madudu kwani anaemaliza alikuja na gea hiyo leo kila kijana wakipindi kile anajuta kasoro wewe uliyepewa unaibu waziri.

Gration Yolonimo: Nadhani January si aina ya vijana wanaoweza kuleta mabadiliko kwa taifa hili lililokwama kwenye tope zito la mfumo mbaya wa utawala. Labda anapima hali ya hewa tu.

Ocol Francis Francis: Tanzania tunahitaji fikra mpya zitoke nje ya ccm maana kama wewe ni kijana unayetaka kugombea uraisi ili kuleta mabadiliko gan? maana kama suala la kupingana na ufisadi umeshindwa xaxa wewe ni kijana au mzee wa kifikra na pili umeshindwa kutetea maoni ya wananchi kwenye katiba mpya je kweli wewe ni kijana mwenye kupenda mabadiliko au ndo kutukejeli wa tz kutuona hatujitambui?kwa maoni yangu kabla hujaanza kutueleza sisi vijana wenzako ili tukusupport anza kujitoa ndan ya ccm maana hatuna iman na ccm 7bu imeshindwa kupambana na ufisadi mf billion 200,ujangil na madawa ya kulevya. pili ungana na ukawa kutetea maoni ya wananchi katika rasimu ya katiba mpya maana yaliyomo ndan ni maon ya watanzania nasio maoni ya makada wachache walioenda dodoma kula pesa za wananchi maana ukishindwa kutetea maon ya wananchi halafu unataka kuleta fikira mpya kweli we kijana mwenzangu,tatu jitafakari na ujipime na ukifanya yote hayo nakupa big up, UJANA NI FIKRA NA MAWAZO MAZURI NA SIO UMRI MKUU.

Mike Nyambi: Makamba mpaka apo tujivunie nn toka kwako?? Mwangalie Magufuli afu jitazame nawewe!

Nasibu Mwailuka: Makamba huyu ninae mfahamu ndiye mwenye hii post? Sasa ngoja nikufunze kwamba hauongozi mbumbu unaongoza raia wenye akili hata kukuzidi wewe, hapa hatuitaji Rais mtoto wala mzee wala Kijana bali tunaitaji Rais mwenye ethics za uongozi mwenye mtazamo wa kimapinduzi ya kimaendeleo. Hivyo kama mzee au Kijana au mtoto anaethics za maitaji ya Watanzania anatufaa.

Smith Lema: Ina maana kwa sasa ukikosa kuteuliwa hutokuja kugombea ukiwa mtu mzima?na mtu mwenye miaka 40 kujiita kijana ni sawa na kutetea mawazo ya kakundi kadogo ka wababa wanaojiita wavulana .tunataka sera na sio ubabaishaji na cha kushangaza hiyo nafasi uliyopewa ya unaibu hujaifanyia chochote cha ajabu .cha msingi mwakani rudi Bumbuli.

Mahfoudh Khamis: Tatizo la Tanzania sio vijana kupewa nafasi kwan hata kama 2kipewa hizo nafasi ha2wezi kuziendesha kama sheria zinavotaka bali tutaendesha kwa matakwa ya watu fulani kwani nchini mwetu hatuna kiongozi mwenye maamuzi ya mwisho kila mtu ni kiongozi kutokana na hela yake ama wadhifa alionao serikalini, kinacho nishangaza ni hiki katiba yetu inasema ''no one is above the law accept the president of urt'' lakin ktk utekelezaji ni kuwa ''no one is above the law accept money'' kuleta mabadiliko tz labda 2we na kiongozi ambaye atakua dikteta ama wakoloni warudi kututawala ndio tz itapiga hatua angalau lakin kwa viongoz hawa akina kikwete, ww makamba, lowasa, slaa, mbatia, lipumba, pinda wote ndo wale wale wenye lengo la kujinufaisha wao na familia zao na kuwaacha watz ktk maisha ya dhiki kama watumwa ktk taifa lao.

Amani Luhuha James: Acha kujipigia debe sema unataka tonge liingie mdomoni izo qualification zimezoeleka unazozisema ndizo makampuni mengi hutumia hata serikali yako hutumia swala ilo la uzoefu. kama umeona ilo ni tatizo umechukua hatua gani kupambana na ilo swala. vijana wengi wanakosa kazi kwa kukosa uzoefu alafu ujatetea chochote leo unataka uraisi ndo unasimama? eti kisa limekugusa ww si vizuri.

Godfrey Bakuza: Sawa kabisa asante MUNGU kwa kunipa nafasi ya kunena juu ya jambo hili. siasa ya tanzania ni uozo mtupu hata wakipaka marashi.maana hata vijana wataoshika nyazifa za uongozi ni watoto wa viongozi waliopita ambapo watafanya kazi kwa matakwa ya baba zao. maana serikali yetu nahisi ina laana maana sauti za wanyonge zimelalama juu ya maovu yanayofanywa na vigogo na akikimbilia kwenye vyombo vya sheria anapingwa tarehe hata wakati mwingine anahatarisha maisha yake sasa hata aongoze kijana au mzee wote ni "EVIL GENERATION"mkombozi wa taifa lako ni wewe mwenyewe na mleta mabadiliko ni wewe mwenyewe.kwanza hata sitaki kusikia maneno ya wanasiasa yaliyojaa tamaa,hila,fitina,elimu kifo na inayonuka. MUNGU NDO SERIKALI YANGU.na neno la mwisho nawatakia wakiliishi mavuno mema ya pesa za wanyonge katka bunge la katiba linalo fuata maana kule ni uchafu tu.

Jabir Shekomba: Kuwa kijana sio kigezo cha wananchi kukuchaguwa kuwa rais, kigezo ni uwezo ulionao wa kuchukuwa maamuzi mazito ktk nchi hii iliyojaa ufisadi wa wazizi,mikataba mibovu isiyo hitaji hata kuwa mwanasheria kugunduwa uozo wake.
Historia yako ktk nafasi ulizo pitia kiuongozi umekemea kiasi gani haya maovu ili uwashawishi wananchi kuwa ukishika nafasi kubwa ya urais utapambana na maovu yote hayo. Kumbuka kufungulia bomba mpaka mwisho haitoshi wakati ndoo imetoboka.

Timothy Edgar: Mimi nakusapoti asilimia 100 wakati wa vijana kushika madaraka ndio huu ambao hawakubali achana nao. Mimi kama kijana nimefurahi sana kwa uthubutu wako na inshallah Mungu atawezesha. #TeamJanuaryMakambathefuturepresident.

Julius Mmari Kessy: Tumefika hapa tulipo sababu ya Sera mbovu za Ccm since independence up to date so hoja hapa sio ujana ila kamwe alietengeneza tatizo hawezilitatua so we need to change system then people...

Marcus Kabwella: Tatizo sio Makamba, tatizo ni wapiga kura maana anajua akipitishwa na CCM kugombea atapita tu maana jamaa wanaamini hata ukisimamisha jiwe ukalivika nguo za Yanga atapita tu!

Davidi Peter Mh huyu jamaa kama hayupo serikalini, sijawahi kumsikia hata siku moja akikemea rushwa na ufisadi uliotapakaa kwenye chama chake huu ni unafiki na kauli za porojo ,kasi zaidi na nguvu mpya zimefanya nini?

Erick Kalinga: Kikwete naye alisema kujenga tanzania mpya kwa hari zaiid ,nguvuzaidi na kasi zaidi ,,,,na umeiyona mwenyewe tanzania mpya sasa achane kutuzingua ,,hebu sema kitu tofauti hasa cha kikazi kipya kiukweli...mfano .100% social services , miundombinu ya kisasa , maisha si ya chini ya dolla moja, watoto wa wasio na wazazi ambao sio viongozi au waasisi wa nchi kupata kazi za maamuzi na sio kama wewe wote tunajuwa ni Fadhila za mzee au mambo yale ya kalenga na chalinze ndo ukemee uwe na maamuzi magumu kama baba wa taifa -hayati mwalimu alikuwa akikuita ikulu kama huna roho ngumu unaweza ukakimbia hata huwo unaibu waziri ila ujuwe kuwa tuna kukubari sana wewe na mawazo yako yako poa,,lakini hakikisha Tanzania mpya inapatikana kwa mali asili tuliokuwa nazo na sio mambo ya 10% na kusaini dark-agreement ikulu na mchina au m-marekani ,,,,please we belive on you we need dictatorship change on development of our country ...please understand.

Godfrey Pius: Binafsi naona bado unacheza nakmbka hayat baba wa taifa alitamka kuwa kiongoz bora atatka ccm na akusema kuwa atakuwa kijana

Damas Kosmas: Sifa ya mtu kuwa kiongozi sio ujana au uzee bali ni hekima na kujitambua,mtu anawezakuwa ni mzee akawa na mitazamo,hekima kama kijana,pia mtu anaweza kuwa ni kijana mtazamo wake ukawa wa kizee hivyo mh #January huna hoja ya msingi!

Palm Kinabo: Ndiyo Wale wale tu ukoo wa panya. Kwakweli hawa watoto wa vigogo msiwape nchi kwakutegemea mabadiliko wanapaka maneno rangi tu ndugu zangu. Tumechomaka name ulaghai wao.

Godfrey Lyimo: Umepewa nafasi kubwa (Naibu Waziri) kipi kipya tumekiona? Nini umetufanyia vijana? Taifa hili linataka fikra mpya kiutendaji sio umri. Umeonyesha utendaji wa Kawaida. Baraza la Mawaziri tulilonalo anayeweza kusimama kwa ushawishi wa fikra mpya ni kutoka wizara ya Uchukuzi na Miundombinu, hawa wamethubutu. Bro tunahitaji Taifa litoke tulipo na kuingia ktk uchumi wa gesi na Rais mtendaji. Kikwete ametoa fursa kubwa kwa vijana kama January lkn ukweli wametuangusha coz bado wazee ambao Wizara zao nimezitaja hapo juu wametuonyesha mengi yanawezekana kama tutawajibika.

Godfrey Manyasi: Jamani tusidanganyane, makamba hata alale uchi(mitambiko), hawezi kuongoza nchi hii, yaani hata ccm wakipiga debe usiku kucha...HAWEZI...let's not waste time on papers and elsewhere..he is incapable in any sense.

Mathew David: Vjana wa anasa,ambao wengne wamepewa huku tukiambiwa wakat wa kuwatumia wananch wao,wako gest na wapenz wao,wapo kwenye bar,vjana wa wanaowatukuza mafsad huku wakiwamwagia matope walala hoi kwa magar ya zawad za watafuna nchi.Huku mkishawishiwa na propaganda za kila mwaka kukopa nje ilikuleta maendeleo kwa wananch.Ingekuwa hivyo nyerere angekopa mpaka basi maana aliichukua nch ikiwa maskn kabsa.
cha msingi hapa vijana watengenezwe kwa ajili ya uongozi si kama walivyo sasa majambazi wa mali ya umma. Hawaridhiki na mishahara yao kazi kudhurumu fedha za miradi kurundikiana posho na chai wakat wadogo zao kijijini wanakaa chin darasani.
Yeye Makamba ni kijana tena mwenye cheo kikubwa tu kama kweli anauchungu na nchi
kwanini hajawahi kukemea mambo hayo? HATUDANGANYIKI!!

Hassan Ibrahim: Kila wakati mtu bora ni anaefikiria kitu mbadala ktk kupata ubora zaidi, kauli ya uzoefu imekua kifuniko kwa harakat za hatam ya vijana ktk kuongoza, lkn hazina ya fikra mpya iko ndani ya vijana ktk heshma ileile ya uasisi wa wazee wetu na uongozi wao. Ndo mana bado mawazo na ushauri wao utahitajika wkt maendeleo yakisukumwa na viongozi vijana wenye uthubutu. Shukran mheshmiwa.

Thomas Yusuph: Taifa hili ni sawa na kibatari kinachoonesha kuishiwa na mafuta, moshi umezidi.ni nguo yenye viraka kibao, ni mgonjwa aliechomwa sindano kila mahali na hajapata nafuu hata kidogo ndani ya miaka 50 ya uhuru,hata kasi mpya imepita hivihivi bila jipya, je ya umri/rika inaweweza kututoa kwenye tope hili la umasikini na ongezeko la deni la taifa?. Tunataka kiongozi atakaye promote accauntability, rule of law, peace and harmony, atakaye tambua degree of political consensus. Tuijenge Tanzania yetu yenye rasilimali rukuki zinazoishia mikononi mwa wasiowazalendo wenye kutaka kuzidi kujilimbikizia tena bila hata haya.

Charle Meena: Kweli kaz ipo kwa watanzania kuacha vyama na kuangalia uwezo na udhubutu wa mtu binafsi kwamaana sote runajua mambo yanayoisibu tz
Tukisema makamba ni mtoto wa kiongozi sawa je km anauwezo na nia ya wa kutuongoza tumpe.

Davie de Mwaky: Mkimaliza umri hamieni kwenye dini, ukanda, urefu, rangi, unene... maana sipaoni ni wapi mtakapochora mstari katika hili.

Shabani Jaka: January ukweli hauepukiki lakini nyuma ya vijana waliofanya mabadiliko kulikuwa na wazee waliokuwa na busara yakafanyika mabadiliko ya maana au mageuzi ya maana isije ikawa history ikaja wahukumu vijana wa kizazi hiki hapa nchini uongozi si mchezo hasa kwa nchi inayoendelea kama yetu.

Teddy Harlison: Uadilifu, kujituma, umakin, nidhamu, utu wema na uzalendo wa watanzania viwe vgezo vya kupata kiongoz bora hususan awe mwenye kujali utu na mwenye kujali taifa lake na raia xo kurithshana kihorela , , hvyo bac umri syo xadifu wa hayo ulosema mh...

Mohamed Makallah: Ndugu zangu wengine kama hatujaelewa mada iliyotolewa na mtoa mada si lazima tuchangie,matusi na kejeli havina nafasi hapa.pia tunashindwa kuelewa niwakati wa vijana kuongoza si uraisi pekee bali kuna mashirika na taasisi (TRA TANESCO BANDARI NK) nyingi za serikali zikiwa na vijana waadilifu wachapa kazi tutafika maana zina mchango mkubwa wa maendeleo kwa nchi yetu so tuache siasa.
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: