Na Hellen Kwavava wa Kajunason Blog.

Jeshi la polisi kanda maalum limefanikiwa kuwakamata majambazi 10 mmojawapo akiwa mwanamke na hiyo imetokana na msako mkali unaoendelea jijini Dar es Salaam.

Majambazi hao wamekamatwa na silaha tisa pamoja na risasi 71 moja katika hizo silaha iliwahi kutumika katika vita yadunia ya kwanza na ya pili.

Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam kamanda wa Polisi kanda maalum Suleiman Kova amesema kwamba watuhumiwa hao wamepatikana kutokana na ushirikiano uliopo kati ya polisi na wananchi.

Aidha kamanda Kova amesema wanatarajia kuimarisha ulinzi mkali katika sehemu zote zitakazofanya ibada ya kusherehekea sikukuu ya Idi alfitri ambayo inatarajia kufanyika kesho.

Hata hivyo amezidi kutoa ushauri katika mabenki yote nchi kuweka camera za cctv au kifaa cha tahadhari kitakachotoa ishara pindi uhalifu unapotaka kufanyika.
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: