Sehemu ya wafanyakazi wa Kikosi zimamoto wakiendelea na zoezi la kuzima moto ulioteketeza kabisa Soko la Ilala Mchikichini Jijini Dar es salaam leo.Moto huo ulianza majira ya saa sita usiku wa kuamkia leo na kuteketeza kila kilichokuwepo katika eneo la soko hilo. Chanzo cha kutokea kwa moto huo bado hakijajulikana mpaka sasa. Picha zote na Othman Michuzi.
 Kazi ya kuzima moto ikiendelea.
 Jitihada za kuuzima moto huo bado zinaendelea.
 Moto bado unaendelea kuwaka mpaka wakati huu,huku jitihada mbali mbali za kuuzima moto huo zikiendelea.
 Baadhi ya wafanyabiashara na mashuhuda wa tukio hilo wakiangalia huku wakiwa hawajua la kufanya,maana mali zote zimeteketea kwa moto huo.
 Soko loote limeteketea kwa moto huo.
 Sehemu ya wafanya Biashara wa soko hilo,wakimuangalia mmoja wa wamachinga akipanga nguo kwenye kibanda chake alichokuja nacho huku wenzie wakiendelea kusikilizia machungu ya kuunguliwa na mali zao.
 Mijadala ya hapa na pale huku moto ukiendelea kuwaka.
 Moja ya cherehani kilichookolewa kutoka ndani ya soko hilo.
 Hivi ndhivyo hali ilivyo katika soko la Ilala Msikichini jijini Dar es salaam leo.
 Hii inaitwa kufa kufaana,jamaa akitafuta waya kwa akili ya kwenda kuuza kwenye vyuma chakavu.
 Usalama kwa watembea kwa miguu hauko vizuri sana,kwani chupa nyingi zimepasuka na kusambaa kila mahali.
 Mabomba yamepinda kutokana na moto huo.
 Moto huo uliteketeza mpaka nguzo za Umeme.
 Baadhi ya mafundi wa kushona nguo wakijadiliana jambo baada ya kuokoa sehemu ya vifaa vyao vya kazi.
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: