MKE wa Rais, Mama Salma Kikwete, anatarajia kuwa mgeni rasmi katika Sherehe za maadhimisho ya Siku ya Wakunga Duniani, zinazotarajia kufanyika Mei 5, jijini Dar es Salaam.
Chama cha Wakunga Tanzania (TAMA) kitaadhimisha siku ya Wakunga Duniani (International Day of Midwives hapa nchini kwa siku mbili kuanzia tarehe 4hadi 5/2015.
Siku ya Wakunga Duniani huadhimishwa duniani kote tarehe tano mwezi wa tano ya kila mwaka.
Madhumuni ya Maadhimisho hayo ni kuhamasisha Wadau mbalimbali pamoja na Jamii kwa ujumla kuhusu umuhimu wa wakunga na shughuli wanazozifanya katika kupunguza vifo vya akina mama vinavyotokana na uzazi pamoja na vifo vya watoto wachanga na wenye umri chini ya miaka mitano.
Kauli Mbiu ya Mwaka huu (2014) ni “Wakunga Wataalam Wanahitajika Duniani kwa wingi sasa kuliko siku zote.” (The World Needs Midwives Today Than Ever)
Hii inalenga katika kuhakikisha kuwa huduma za Afya ya Uzazi na Mtoto zinatolewa na Wakunga wenye utalaam kwa kufuata miongozo na viwango vilivyowekwa ili kuchangia katika kufikia Malengo ya Maendeleo ya Milenia namba 3,4, 5 na 6.
Tanzania ni mmojawapo ya nchi zenye uhaba wa watao huduma wenye ujuzi hususani Wakunga katika ngazi ya zahanati na vituo vya afya ambako ndiko wakinana mama wengi wanapata huduma ya wakiwa wajawazito, kujifungua na baada ya kujifungua.
Katika kuadhimisha siku hiyo, Wakunga kwa kushirikiana na wadau mbalimbali watafanya shughili tatu ambazo ni:
1. Kongamano la kisayansi kwa siku moja tarehe 4/5/2014 ambapo watajadili mada na shughuli mbalimbali zinazofanywa na Wakunga.
Mahali : Hospitali ya Taifa ya Muhimhili Jengo la New OPD Chumba no 60, linaloangaliana na Wadi ya Wazazi.
Mgeni Rasmi: Mheshimiwa Dkt. Seif S Rashidi (MB) Waziri wa Afya na Ustawi Wa Jamii.
2 Kutoa huduma za afya ya uzazi na mtoto katika viwanja vya Mnazimmoja kwa akina mama, watoto , vijana na wanaume kwa siku mbili 4/hadi 5/2014. Huduma zitakazotolewa ni:
* Uzazi wa mpango,
* Chanjo kwa watoto
* Ushauri na upimaji wa hiari wa virus vya UKIMWI,
* Uchunguzi wa saratani ya matiti na kizazi kwa akina mama
* Utoaji wa hiari wa damu.
* Elimu na ushauri kuhusu hudma ya Afya ya Uzazi na Mtoto
* Wanaume watapata sindano ya Pepopunda ( tetanus)
Huduma zitakazotolewa ni bure hakuna malipo.
3 Kufanya mandamano kutoka makao makuu ya Wizara ya Afya hadi Viwanja vya Mnazimmoja siku ya kilele tarehe 5/5/2014. Maandamano yataongozwa na Brass band ya JKT Mgulani.
Mgeni Rasmi ni: Mheshimiwa Mama Salma Kikwete, Mke wa Mh. Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania
Kwa heshima na taadhima Chama kinaomba vyombo vya habari kutusaidia kutoa taarifa kwa Wananchi.
Tunatanguliza shukurani zetu.
Dr Sebalda Leshabari
KATIBU MKUU TAMA
KATIBU MKUU TAMA
Toa Maoni Yako:
0 comments: