Shirikisho la ngumi Tanzania (BFT) linatoa pongezi za dhati kwa Waziri wa Mambo ya Nchi za Nje Mh. Bernard Membe kwa hatua na jitihada alizozifanya za kutafua na kufanikisha kambi ya mazoezi kwa Timu ya Taifa ya ngumi inayojiandaa kushiriki mashindano ya jumuiya ya madola yatakayofanyika July, 2014 Nchini Scotland.
Kwa hakika ni mmoja wa watanzania ambae ameguswa na maandalizi ya Timu yetu ya Taifa kwa kuitafatia kambi ya mazoezi ya kimataifa Nchini Uturuki na Nchini China kwani timu yetu ilikuwa inafanya mazoezi katika hali duni bila ya kuwa na vifaa vya kisasa kulingana na mabadiliko ya mchezo wa ngumi duniani.
Kwa kufanya hivyo tunakuwa na uhakika mkubwa wa kupata medali katika mashindano hayo ya Jumuiya ya Madola na Tanzania kutangazika vema Kimataifa kupitia mchezo wa ngumi maana bado tunakumbuka historia nzuri ya ushiriki waTanzania katika mashindano ya Jumuiya ya madola kwani kwa mara ya kwanza Tanzania ilishiriki mwaka 1972 na Tanzania kupata medali ya kwanza ya kimataifa baada ya Tanzania kupata uhuru, iliyoletwa na Bondia (LYTUS SIMBA) na baada ya hapo baadhi ya mabondia walioleta medali ni kama wafuatao:
MICHAEL YOMBAYOMBA : (Dhahabu)
HAJI MATUMLA : (Fedha)
MAKOYE ISANGURA : (Shaba)
MWAMBEYA BAKARI : (Shaba)
WILLY ISSANGURA : (Shaba)
LUCAS MSOMBA : (Shaba)
Bado BFT tunamuomba azidi kutusaidia vifaa zaidi hasa ulingo wa kisasa na Computer inayotumika kuhesabia point za ushindi wakati wa mashindano kwani Nchi zote duniani ndizo wanazozitumia na niagizo kutoka chama cha ngumi cha dunia kwa wanachama wote lazima waitumie katika mashindano..
Toa Maoni Yako:
0 comments: