Kaimu Mhifadhi wa Mbuga ya Ngorongoro, Bw. Amio Amio ambaye aliyemwakilisha mgeni rasmi katika uzinduzi wa Mbio za Tigo Ngorongoro zilizofanyika jana Aprili 19, 2014 kuanzia Mbuga ya Ngorongoro na kuishia mjini Karatu akiongea machache wakati wa hafla ya kuwakabidhi washindi zawadi zao. Pembeni yake ni Mkurugenzi wa Kanda wa Kampuni ya simu ya mkononi ya TIGO, Brian Kalokola.
Kaimu Mhifadhi wa Mbuga ya Ngorongoro, Bw. Amio Amio (kushoto) na Mkurugenzi wa Kanda wa Kampuni ya simu ya mkononi ya TIGO, Brian Kalokola (kulia) wakimkabidhi zawadi ya shilingi Mil. 1 mshindi wa kwanza wa Mbio za Tigo Ngorongoro kwa kilomita 22 (Half Marathon) kwa upande wa wanaume, Alphonce Felix mara baada ya kunyakua taji hilo kwa kuvunja rekodi kwa kukimbia muda wa 1:03:59. Mbio hizo za Tigo Ngorongoro zilifanyika jana Aprili 19, 2014 kwa kuanzia geti kuu la Mbuga ya Ngorongoro na kuishia mjini Karatu. Tigo ndiyo walikuwa ni wadhamini wakuu wa mashindano hayo,
 Mkurugenzi wa Kanda wa Kampuni ya simu ya mkononi ya TIGO, Brian Kalokola (kulia) akimkabidhi zawadi ya shilingi Mil. 1 mshindi wa kwanza wa Mbio za Tigo Ngorongoro kwa kilomita 21 (Half Marathon) kwa upande wa wanawake, Jackline Sakilu mara baada ya kunyakua taji hilo kwa kuvunja rekodi kwa kukimbia muda wa 1:14:29.
Mwenyekiti mstaafu wa Chama Cha Riadha Tanzania, akitoa zawadi kwa Fabian Joseph aliyeshika nafasi ya nne,
Mwakilishi wa kampuni ya Utalii ya ZARA ambao ndiyo waandaaji wa mashindano hayo akitoa zawadi kwa mshindi wa saba kwa upande wa wanawake.
Washindi wa Mbio za Tigo Ngorongoro upande wa wanawake wakiwa wamejipanga kusubiri zawadi zawadi zao… kutoka kulia mshindi wa kwanza Jackline Sakilu, Nathalina Elisante, Marry Naali, Failuna Abdi na Flora Yuda.
Wanariadha wa Mbio za Tigo Ngorongoro Kilometa 21 (Half Marathon) wakianza mbio katika geti kuu la Mbuga ya Ngorongoro na kuishia mjini Karatu.
Mchuano wa wanariadha ukiendelea kwa kasi.
Ilikuwa ni patashika nguo kuchanika kila mmoja akitaka kuchomoza ili aweze kushinda.
Mshindi wa kwanza wa Mbio za Tigo Ngorongoro kilomita 21 (Half Marathon) kwa upande wa wanaume, Alphonce Felix akiwachomoka wenzake.
Mshindi wa kwanza wa Mbio za Tigo Ngorongoro kwa kilomita 21 (Half Marathon) kwa upande wa wanaume, Alphonce Felix akimaliza kwa furaha.
Mshindi wa kwanza wa Mbio za Tigo Ngorongoro kwa kilomita 21 (Half Marathon) kwa upande wa wanawake, Jackline Sakilu akimaliza mbio.
Umati wa Wakazi wa Mji wa Karatu wakifuatilia michuano hiyo.
Hapa ndipo kulipoanzia kwa mbio za makampuni... ambapo makampuni yalikimbia kilometa 5.
Mshindi wa kwanza wa mbio za makampuni akifurahia mara baada ya kumaliza.
Mkururenzi Mtendaji wa Kampuni ya Frontline Porter Novelli, Irene Kiwia hakuwa nyuma kushiriki mbio hizo.
Washiriki wa Mbio za Tigo Ngorongoro Kilometa 5 za Makapuni wakimenyana vikali.
Timu ya Kampuni ya Frontline Porter Novelli ya jijini Dar es Salaam wakiwa katika sura ya furaha mara baada ya kumaliza kukimbia Kilometa 5 katika Mbio za Tigo Ngorongoro.
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: