Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akisalimiana na Mwadhama Cardinari Polycap Pengo, wakati wa ibada maalum ya Harambee ya kuchangia ujenzi wa Ukumbi wa mikutano wa Kanisa la Mtakatifu Peter lililopo Oysterbay jijini Dar es Salaam, leo asubuhi Jan 26, 2014. Picha na OMR
Baadhi ya waumini wa dini ya Kikristu waliohudhuria Ibada hiyo kwenye ibada hiyo.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Bilal, akiongoza na na Rais Mstaafu Benjamin Mkapa, kutoka kanisani baada ya ibada hiyo.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib
Bilal, akisikiliza maelezo kutoka kwa Paroko wa Parokia ya Mtakatifu Peter, Stephano Kaombe, kuhusu maendeleo ya ujenzi wa Ukumbi wa mikutano wa Kanisa la Mtakatifu Peter lililopo Oysterbay jijini Dar es Salaam, wakati wa harambee ya kuchangia ujnenzi wa Ukumbi huo iliyofanyika leo asubuhi Jan 26, 2014. Picha na OMR.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akizungumza na Rais Mstaafu wa awamu ya tatu, Benjamin Mkapa wakati alipotembelea kukagua maendeleo ya ujenzi wa ukumbi wa mikutano wa Kanisa la Mtakatifu Peter, baada ya ibada maalum ya harambee ya kuchangia ujenzi huo, iliyofanyika leo asubuhi, Jan 26, 2014. Kushoto ni Paroko wa Parokia ya Mtakatifu Peter, Stephano Kaombe. Picha na OMR
Picha ya pamoja....
---
Zaidi ya shilingi milioni 65 zimekusanywa katika harambee iliyoongozwa na Makamu wa Rais Dkt. Mohammed Gharib Bilal kwa ajili ya kuchangia ujenzi wa ukumbi wa mikutano wa Kanisa la Mtakatifu Peter lililoko jijini Dar es salaam.

Kati ya fedha hizo zilizokusanywa katika ibada maalum ya kuchangia ujenzi wa jengo la ukumbi huo ilyoongozwa na Mhadhama Kadinali Polycap Pengo kiasi cha shilingi milioni 60.5 zilikuwa ni ahadi na shilingi milioni 5 zikiwa ni fedha taslimu.

Akizungumza katika hafla hiyo, Makamu wa Rais aliwahakikishia Watanzania kuwa serikali itaendelea kuunga mkono juhudi za taasisi za kidini katika kudumisha amani na upendo ndani ya jamii bila ya kujali tofauti za aina yo yote ile.

Alisema kuwepo kwake katika hafla hiyo ni ishara ya uhusiano mkubwa uliokuwepo kati ya serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Taasisi mbali mbali za dini nchini.

“Sisi Watanzania tumefika hapa kutokana na uongozi thabiti wa waasisi wa Taifa letu. Hivyo, tunataka nchi ya watu wanaomwogopa Mungu, watu wanaopendana, watu wanaovumiliana na watu wanaotakiana mema katika shughuli zao.”

Kwa mujibu wa Mwenyekiti wa Kamati ya Ujenzi, Bibi Rose Rupia kamati yake inahitaji shilingi milioni 600 zaidi kukamilisha hatua za mwisho za ujenzi wa jengo la ukumbi huo na kwamba tayari wameshatumia kiasi cha shilingi bilioni moja katika ujenzi huo.

Ibada hiyo maalum ilihudhuriwa pia na viongozi mbali mbali akiwemo Rais Mstaafu wa Awamu ya Tatu Benjamin William Mkapa.
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

1 comments: