'Aliyekuwa Naibu Katibu Katibu Mkuu' wa Chadema, Zitto Kabwe (kulia) akizungumza kwa hisia wakati alipokuwa akitoa tamko rasmi kuhusu 'maamuzi magumu', yaliyochukuliwa na chama chake kwa kuvuliwa madaraka ya ndani ya chama hicho kwa kile kilichoelezwa kuihujumu Chadema.

Zitto Kabwe na Kitila Mkumbo wakiingia Ukumbini katika Hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam, mchana huu kwa ajili ya kuzungumza na waandishi wa habari.
Zitto Kabwe (kulia) na Dk. Kitilla Mkumbo, wakisikiliza kwa makini maswali yaliyokuwa yakiulizwa na waandishi wa habari wakati wa mkutano huo.
Viongozi wakiwa makini katika kusikiliza maswali.......
Zitto Kabwe, akiagana na baadhi ya waandishi wa habari wakati akiondoka ukumbini.
---
Na Mwandishi Wetu

MBUNGE wa Chadema na Naibu Kiongozi wa Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni, Zitto Kabwe amefunguka na kusema hayupo tayari kuondoka katika chama cha Chadema mpaka watakapoanza wao wanaomchokonoa kuanza kuondoka.

Zitto amesema hayo leo katika mkutano na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam alipokuwa anazungumzia maamuzi ya Kamati Kuu ya Chadema ya kumvua nafasi zake zote za uongozi yeye pamoja na Mjumbe wa Kamati Kuu ya chama hicho Dk. Kitilla Mkumbo na aliyekuwa Mwenyekiti wa Chadema Mkoa Arusha Samson Mwigamba.

Zitto amekana kuhusika wala kuujua waraka wa siri ambao ndiyo uliosababisha kumvua madaraka baada ya uamuzi wa Kamati Kuu ya chama kuunasa waraka huo.

"Mimi nimeusikia ule waraka kwa mara ya kwanza kwenye Kamati Kuu na nilisikitika sana kwanini hukunifikia haraka kwani ningeanza kutekeleza mara moja." alisema Zitto akizungumza.

Huenda leo watu walitegemea nitafanya maamuzi magumu ya kuondoka kwenye chama; "Mimi bado ni mwanachama wa Chadema na nitakuwa wa mwisho kutoka kwenye chama hiki kwa hiyari yangu, nitafanya taratibu zote za chama kuhitimisha jambo hili mimi sitoki kwenye chama hiki labda wanitoe wao," alisema Zitto.

Zitto amesema anaumia anapotuhumiwa kwa kuwa yeye ni binadamu. "...ninapotuhumiwa naumia ninapoambiwa naujumu chama hiki naumia kwa kuwa nakipenda chama na nimekitumikia muda mrefu. Aidha aliwataka viongozi wa Chadema kuacha siasa za uzushi ili kujenga chama himara na kuwakomboa Watanzania.

"...Sisemi kama mimi sina makosa ni binadamu nimefanya mambo mengi kwa chama changu, lakini kinachoendelea kwa sasa ndani ya chama chetu ni mapambano ya kukuza demokrasia na ni mapambano ya wanaotaka mabadiliko na wasiopenda mabadiliko ndani ya chama... mapambano ya wawajibikaji na wasiopenda kuwajibika ni mapambano ya wanaopenda demokrasia na wanaokwaza demokrasia." alisema Zitto.

Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

2 comments:

  1. naamin chama hakijakurupuka kufanya maamuzi ya kuwavua uanachama na ndio maana wamejiridhisha kwamba zitto u don deserve 2 be a follower in chadema

    ReplyDelete
  2. Kina Zitto wako sahihi, Mbowe na Slaa jibuni hoja! Kaeni mezani mjadiliane

    ReplyDelete