Mkurugenzi wa Airtel Tanzania, Bw. Sunil Colaso akielezea jinsi Airtel inavyowathamini wateja wake kwa kuwawezesha kushinda tiketi za kuweza kujionea mechi mojawapo ya Timu ya Manchester United.
 Baadhi ya wadau mbalimbali wakifuatilia kwa umakini uzinduzi wa promosheni hiyo mpya ya ‘MIMI NI BINGWA’ uliofanywa na Airtel Tanzania kwa ushirikiano na klabu ya Manchester United.
 Meneja Uhusiano wa Timu ya Manchester United, Bw. Michael Higham akielezea faida za muungano kati ya Airtel Tanania na Manchester kuwa utaongeza hata idadi ya mashabiki wa klabu hiyo kwa Watanzania.
 Mkurugenzi wa Kitengo cha Masoko kutoka Airtel Tanzania, Bw. Levi Nyakundi (kushoto) akiwa pamoja na Mkurugenzi wa Kitengo cha Masuala ya Fedha Airtel Tanzania, Bw. Kalpesh Mehta wakifuatilia kwa umakini kabisa uzinduzi wa promosheni hiyo mpya.
 Mtangazaji wa Clouds FM, Ephraim Kibonde ambaye alikuwa ni mshehereshaji wa uzinduzi wa promosheni ya ‘MIMI NI BINGWA’ akizungumzia promosheni mpya ya Airtel iliyozinduliwa jana katika hoteli ya Hyatt Regency jijini Dar es salaam. Kutoka kulia ni Rais mpya wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), Jamal Malinzi, Mkurugenzi wa Maendeleo ya Michezo, Bw. Leornad Thadeo, Mkurugenzi wa Airtel Tanzania Sunil Colaso pamoja na Meneja Uhusiano wa Timu ya Manchester United, Bw. Michael Higham.
 Mkurugenzi wa Airtel Tanzania, Bw. Sunil Colaso akimkabidhi jezi ya Timu ya Manchester United Mkurugenzi wa Maendeleo ya Michezo Bwana Leornad Thadeo jezi mpya ya Manchester United.
 Mkurugenzi wa Airtel Tanzania, Bw. Sunil Colaso akimkabidhi jezi ya Timu ya Manchester United, raisi mpya wa shirikisho la mpira wa miguu Tanzania Bw. Jamal Malinzi.
Mkurugenzi wa Airtel Tanzania, Sunil Colaso akimkabidhi jezi ya Timu ya Manchester United mtangazaji wa Clouds FM, Bw. Ephraim Kibonde ambaye alichukua kwa niaba ya wapenzi wa mpira.
 
Mkurugenzi wa Airtel Tanzania, Bw. Sunil Colaso (wa pili kutoka kushoto) akiwa pamoja na Meneja Uhusiano wa Timu ya Manchester United, Bw. Michael Higham (wa kwanza kushoto). Kutoka kulia ni Mkurugenzi wa Maendeleo ya Michezo, Bw. Leornad Thadeo, Rais mpya wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), Jamal Malinzi na Mtangazaji wa Clouds FM, Bw. Ephraim Kibonde muda mfupi baada ya uzinduzi wa promosheni ya ‘MIMI NI BINGWA’ iliyofanyika katika hoteli ya Hyatt Regency jijini Dar es salaam.
---
*Wateja wa Airtel 10 kila mwezi kushinda tiketi za kwenda Old Trafford kushuhudia mechi LIVE

KAMPUNI ya mawasiliano ya Airtel Tanzania imetangaza ushirikiano na klabu nguli ya mpira wa miguu ya Manchester United ya nchini Uingereza utakaowezesha wateja wa kampuni Airtel 10 kila mwezi kujishindia safari za kwenda kushuhudia mechi za klabu hiyo moja kwa moja (live) katika uwanja wa Old Trafford.

‘Mimi Ni Bingwa’ inalenga kuwazawadia wateja zawadi zenye thamani za zaidi ya shilingi milioni 500.

Akizungumza wakati wa hafla ya uzinduzi wa promosheni Mkurugenzi Mtendaji wa Airtel Tanzania, Sunil Colaso alisema ubia huo mpya unadhihirisha nia ya kampuni ya kufurahisha na kutosheleza mahitaji ya wateja wake.

“Kampuni ya Airtel Tanzania tunaingia ubia mpya na klabu ya Manchester United ambao utawapa na nafasi wateja wetu wote na wapenzi wa Mpira fursa za kuangalia mechi za timu ya Manchester United live katika uwanja wa Old Trafford.



“ Natoa wito kwa wateja wetu kuchangamkia fursa hii na kushiriki kikamilifu ili kujishindia zawadi mbali mbali za kila siku, kila wiki na zawadi nono ya shilingi milioni 50 itakayotolewa mwishoni mwa promosheni hii,” aliongeza.



Aidha Colaso alisema kuwa kampuni yake imekuwa chachu ya maendeleo ya michezo mbali mbali ikiwemo mpira wa miguu kupitia mkakati madhubutu wa kuendeleza mpira wa miguu maarufu kama Airtel Rising Stars.



“Tunajivunia kuwa mpango wetu wa Airtel Rising Stars imeanza kuvumbua vipaji nchini Tanzania na barani Afrika kwa ujumla. Pia tunajivunia kuwa Tanzania imefanya vizuri katika mashindano ya Airtel Rising Stars ya Afrika ya vijana chini ya miaka 17 yaliyofanyika nchini Nigeria miezi michache iliyopita,” aliongeza.



Naye, Meneja Mahusiano wa Klabu ya Manchester United Michael Higham wakati wa hafla hiyo alisema ubia wa klabu yake na kampuni ya Airtel ya Tanzania umelenga kuongeza uwakilishi wa klabu hiyo nchini Tanzania.



“Tunafaraja kupata ubia huu mpya na tuna matumaini kuwa hii itakuwa fursa nzuri ya kuwapatia na kujionea mechi kali moja kwa moja. Bila shaka, tunategemea kuwa ushirikiano huu utatusaidia kuongeza mashabiki hapa Tanzania,” alisema Higham.



Aidha, Mkurugenzi wa Idara ya Maendeleo ya Michezo wa Wizara ya Habari, Vijana Utamaduni na Michezo, Leonard Tadeo wakati wa hafla hiyo aliipongeza kampuni ya Airtel kwa kuendelea kusaidia maendeleo ya sekta ya michezo nchini.

“Nachukua nafasi hii kuishukuru kampuni ya Airtel Tanzania kwa jitihada zake za kuendelea kusaidia maendeleo ya michezo nchini hususani Airtel Rising Stars ambayo imeibua vipaji kama Serengeti Boys na Timu ya Tanzanite kwa wasichana ambao wamekuwa wakiiwakilisha nchi vizuri katika michezo ya kimataifa,” alisema Tadeo.

Wakati huo huo, Rais wa Shiriko la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), Jamal Malinzi wakati wa tukio hilo naye aliishukuru Airtel kwa uhusiano wake wa muda mrefu na shirikisho na kuyaasa makampuni mengine kusaidia maendeleo ya michezo nchini.

“Kampuni ya Airtel Tanzania imekuwa ni chombo muhimu katika maendeleo ya michezo ikiwa ni pamoja na mpira wa miguu kupitia mpango wake wa Airtel Rising Stars ambao umetuletea heshima kubwa kimataifa miezi michache iliyopita.

“TFF itaendelea kufanyakazi kwa ukaribu na wadau mbali mbali ili kuhakikisha tunaupeleka mchezo wa mpira wa miguu nchini katika ngazi ya juu zaidi,” alisema.

Zawadi za thamani ya zaidi ya milioni 500 zitashindaniwa katika promosheni ya ‘Mimi ni Bingwa’ na Airtel Tanzania.

Washindi katika promosheni hiyo watajishindia jezi halisi za timu ya Manchester United, fedha taslim kila siku na kila wiki na zawadi kubwa ya shilingi milioni 50 mwishoni mwa promosheni.

Ili kushiriki kwenye promosheni ya Airtel MIMI NI BINGWA mteja anatakiwa kutuma ujumbe mfupi (SMS) ukiwa na neno “BINGWA” kwenda namba 15656 .
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: