Msanii wa Muziki wa Kizazi Kipya, Selemen Msindi a.k.a Afande Selle mapema leo atapokea kadi ya uanachama wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kupitia kata ya Misufini ikiwa njia ya kujitayarisha kugombea jimbo la Morogoro mjini mwaka 2015 kupitia chama hicho.
Akizungumza na mtandao huu Afande Selle alisema kuwa leo Jumapili Nov 17 kuna mkutano mkubwa wa Chama cha CHADEMA katika kata hiyo ya Misufini ambapo viongozi mbalimbali akiongozwa na Mbunge wa Nyamagana, Jijini Mwanza, Ezekiel Wenje watakuwepo katika mkutano huo.
Mapema mwaka huu Afande Selle alitangaza kugombea ubunge jimbo la Morogoro mjini bila kubainisha Chama husika.
Toa Maoni Yako:
0 comments: