Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari Vijana,
Utamaduni na Michezo Prof. Elisante Ole Gabriel akitoa somo kwa vijana
kutoka maeneo mbalimbali nchini kuhusu namna wanavyoweza kutumia fursa
zilizopo kupambana na umasikini na tatizo la ajira wakati wa mdahalo wa
Wiki ya Vijana leo mkoani Iringa.
Mbunge wa jimbo la Mchinga Mh. Saidi Mtanda akizungumza na Vijana wakati wa mdahalo leo mkoani Iringa.
Picha ya pamoja.
Picha/Habari na Aron Msigwa -MAELEZO.
Vijana kote nchini wametakiwa kuacha tabia ya
kulalamika na badala yake wazitumie
fursa za kiuchumi zilizopo katika maeneo yao kubuni miradi mbalimbali na kufanya
kazi kwa bidii ili jamii iweze kuwaheshimu
na kuthamini mchango wao.
Akizungumza na vijana wakati
wa mdahalo wa vijana uliofanyika katika chuo cha Ufundi (VETA) mkoani Iringa
leo, Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Habari
Vijana, Utamaduni na Michezo Prof. Elisante Ole Gabriel amesema kuwa vijana ndio
nguvu kazi ya taifa hivyo hawapaswi
kulalamika badala yake washiriki kikamilifu katika kupambana na tatizo la
ukosefu wa ajira kwa kuyatumia mazingira yanayowazunguka.
Amesema kuwa tatizo la
vijana wengi Tanzania kukabiriwa na changamoto ya ukosefu wa ajira hasa maeneo
ya mijini linatokana na wengi wa vijana kushindwa kubaini fursa za ajira
zilizopo katika mazingira wanayoishi hivyo kuishia kuilaumu serikali.
Amesema vijana wengi wanakosa moyo wa kuthubutu kuingia katika
biashara halali za kuweza kuwapatia kipato na kujikuta wakitumia muda mwingi
kukaa viweni na kusubiri serikali iwatafutie ajira jambo ambalo linachangia
vijana wengi kuendelea kuwa maskini.
“Ifike mahali tukubali
kuwa hakuna changamoto yoyote duniani ambayo siyo fursa,hapa Tanzania yapo
maeneo mengi ambayo vijana mkikaa vizuri mnaweza kutajirika"
Toa Maoni Yako:
0 comments: