Pichani ni kamanda wa Polisi Mkoa wa                                   Mbeya, DIWANI ATHUMANI - ACP

WILAYA YA  CHUNYA – KUPATIKANA NA SARE ZA  ASKARI WANYAMA PORI NA PINGU.
MNAMO

TAREHE 18.10.2013 MAJIRA YA  SAA 13:00HRS HUKO KATIKA KIJIJI CHA
BITIMANYANGA, KATA YA  MAFYEKO, TARAFA YA KIPEMBAWE WILAYA YA  CHUNYA
MKOA WA MBEYA.  ASKARI POLISI WAKIWA DORIA/MSAKO  KWA KUSHIRIKIANA NA
ASKARI WANYAMAPORI WALIMKAMATA SAMWEL S/O VITALIS @ MANDE , MIAKA 34,
MNYATURU, MKULIMA, MKAZI WA KIJIJI CHA BITIMANYANGA  AKIWA NA SARE PAIR
MOJA “KOMBATI”  ZA ASKARI WA WANYAMAPORI PAMOJA NA PINGU MOJA. MBINU NI
KUTUMIA VIFAA HIVYO KATIKA UWINDAJI HARAMU.  TARATIBU ZA KISHERIA
ZINAFANYWA ILI AFIKISHWE MAHAKAMANI. KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA 
KAMISHNA MSAIDIZI WA POLISI DIWANI ATHUMANI  ANATOA WITO KWA JAMII
KUACHA KUMILIKI MALI ZA SERIKALI  ISIVYO HALALI KWANI NI KOSA LA JINAI.
AIDHA ANAENDELEA KUTOA RAI KWA YEYOTE MWENYE TAARIFA JUU YA  MTU/WATU AU
KIKUNDI KINACHOMILIKI MALI ZA SERIKALI /WAWINDAJI HARAMU AZITOE KATIKA
MAMLAKA HUSIKA ILI  WAHUSIKA WAKAMATWE NA SHERIA ICHUKUE MKONDO WAKE.
WILAYA YA  MBEYA MJINI  – KUPATIKANA NA POMBE HARAMU YA  MOSHI [GONGO].
MNAMO

TAREHE 21.10.2013 MAJIRA YA  SAA 12:00HRS HUKO KATIKA MTAA WA MANGA –
MWANJELWA , KATA YA  MANGA , TARAFA YA IYUNGA JIJI NA MKOA WA MBEYA. 
ASKARI POLISI WAKIWA DORIA/MSAKO  WALIWAKAMATA 1. ITIKA D/O KIMANGA,,
MIAKA 41, KYUSA, MKULIMA, MKAZI WA MWANJELWA 2. YASIWA S/O SHELISHELI,
MIAKA 37, MNYIHA, MKULIMA, MKAZI WA MANGA, 3. MATESO S/O SHELISHELI,
MIAKA 33, MNYIHA,MKULIMA, MKAZI WA CHUNYA NA 4. EMANUEL S/O SILAVWE,
MIAKA 33, MNYAMWANGA, MKULIMA, MKAZI WA MANGA  WAKIWA NA POMBE HARAMU
YA  MOSHI [GONGO] UJAZO WA LITA NANE [08]. WATUHUMIWA NI WAUZAJI NA
WATUMIAJI WA POMBE HIYO.  TARATIBU ZA KISHERIA ZINAFANYWA ILI WAFIKISHWE
MAHAKAMANI. KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA  KAMISHNA MSAIDIZI WA
POLISI DIWANI ATHUMANI  ANATOA WITO KWA JAMII KUACHA KUTUMIA POMBE
HARAMU YA  MOSHI [GONGO] KWANI NI KINYUME CHA SHERIA NA NI HATARI KWA
AFYA YA  MTUMIAJI.


WILAYA YA  MOMBA  – KUPATIKANA NA BHANGI. 
MNAMO

TAREHE 21.10.2013 MAJIRA YA  SAA 05:00HRS HUKO KATIKA MTAA WA MJINI ,
KATA YA  TUNDUMA  , TARAFA YA TUNDUMA WILAYA YA  MOMBA  MKOA WA MBEYA. 
ASKARI POLISI WAKIWA DORIA/MSAKO  WALIMKAMATA 1. EDMUND S/O KANFWA,,
MIAKA 41, KYUSA, MKULIMA, MKAZI WA MWANJELWA NA  2. TAIFA S/O
MWAMAHONJE, MIAKA 22, MMALILA, MKULIMA WOTE WAKAZI WA MIGOMBANI –
TUNDUMA WAKIWA NA BHANGI KETE 18 SAWA NA UZITO WA GRAM 90. WATUHUMIWA NI
WAUZAJI NA WAVUTAJI WA  BHANGI.  TARATIBU ZA KISHERIA ZINAFANYWA ILI
WAFIKISHWE MAHAKAMANI. KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA  KAMISHNA
MSAIDIZI WA POLISI DIWANI ATHUMANI  ANATOA WITO KWA JAMII KUACHA KUTUMIA
DAWA ZA KULEVYA KWANI NI KINYUME CHA SHERIA NA NI HATARI KWA AFYA YA 
MTUMIAJI.
[ DIWANI ATHUMANI - ACP ]
KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA.
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: