Na Flora Mbasha
Mungu wetu, na Baba wa Bwana wetu Yesu Kristo, tunakushukuru kwa ulinzi wako kutwa nzima ya leo. Tunakusihi Ee Bwana, wakati huu, tunapoelekea kulala, uzidi kuonekana kwetu, usituache, wala usiende mbali nasi Ee ngao yetu. Tupiganie dhidi ya adui zetu wanaolenga kutushambulia kupitia ndoto chafu, ugomvi, chuki,kuloga,machuki binafsi, kutokulewana kwenye nyumba zetu!Kwa jina la Yesu Kristo.

Tupe amani na kupendana siku zote. Tujalie furaha yako Ee Baba, na shagwe itawale muda wote.tupe utajiri mana umesema fedha na dhahabu ni mali yako, Uweza wa Roho wako Mtakatifu,uwe kiongozi wetu; Kwa Jina la Yesu Kristo.
Tupe maono mapya, tupe kukupenda, tupe Roho ya kukutumikia, tupe ujasiri na uweza wa kuitambua na kuishinda dhambi. Tupe hekima ya kuzijua njia zidanganyazo na ibada za kipepo, Kwa Jina la Yesu Kristo.
Tupe ufunuo mpya juu ya kazi yako,zidi kutukumbusha kulisoma neno lako na kulitafakari daima, tupe muda wa kukuomba na kukuabudu kama upendavyo Ee Mungu wetu. Rehema zako na Neema yako, iwe juu yetu; Kwa Jina la Yesu Kristo.
Kwa wingi wa hekima yako, tujalie kadri upendavyo, kupitia Roho Mtakatifu, anayetuombea mbele zako daima tena kwa kuugua, hata zaidi tuombavyo. AMEN.
she is right
ReplyDelete