Meneja wa Mauzo ya Rejareja wa Kampuni ya Bia Tanzania (TBL) Kanda la Ziwa, Andrew Mbwambo (kulia) akikabidhi kitita cha Sh. Laki 5 kwa Mshindi wa Kwanza wa Mitindo kwenye Redd's Uni-Fashion Bash, Fahad Rajab (kutoka Chuo cha Mt. Augustine ya jijini Mwanza) baada ya kuwagaragaza wenzake, katika Tamasha lililofanyika kwenye Bustani ya Charcoal Ribs Beach Resort jijini, Mwanza mwishoni mwa wiki.
Meneja wa Mauzo ya Rejareja wa Kampuni ya Bia Tanzania (TBL) Kanda la Ziwa,Andrew Mbwambo (kulia) akikabidhi kitita cha Sh. Laki 7 kwa Mshindi wa Kwanza wa Ubunifu wa Mitindo kwenye Redd's Uni-Fashion Bash,Dotto Elias (kutoka Chuo cha Biashara cha CBE jijini Mwanza) baada ya kuwagaragaza wenzake,katika Tamasha hilo lililofanyika kwenye Bustani ya Charcoal Ribs Beach Resort jijini, Mwanza.
Mshindi wa kwanza wa Miondoko ya Mitindo, Fahad Rajab (pili kushoto) na Mshindi wa pili, Lucy Charles (kushoto) wakifurahia vitita vyao pamoja na wenzao.
Mkali Muziki wa Kufoka hapa nchini, Fareed Kubanda a.k.a Fid Q akitoa burudani kwa wakazi lukuki wa Jiji la Mwanza waliokuwa wamefurika kwa wingi kwenye Bustani ya Charcoal Ribs Beach Resort jijini, Mwanza kushuhudia Tamasha la Redd's Uni - Fashion Bash.
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: