Timu ya mpira wa pete ya Utumishi ikipasha kabla ya kuanza mechi kati yake na RAS Manyara katika viwanja vya Chuo Kikuu Dodoma.
Timu ya mpira wa pete ya utumishi ikiwa tayari kwa ajili ya ukaguzi kabla ya kuanza mechi kati yake na RAS Manyara katika viwanja vya Chuo Kikuu Dodoma.
Timu ya mpira wa pete ya RAS Manyara ikiwa tayari kwa ajili ya ukaguzi kabla ya kuanza mechi kati yake na Utumishi katika viwanja vya Chuo Kikuu Dodoma.
Mechi kati ya timu ya mpira wa pete ya Utumishi na RAS Manyara iliyofanyika viwanya vya Chuo Kikuu Dodoma.
Mechi kati ya timu ya mpira wa pete ya Utumishi na RAS Manyara iliyofanyika viwanya vya Chuo Kikuu Dodoma. Mchezaji wa timu ya mpira wa pete ya Utumishi Elizabeth Fusi (C) akitoa pasi wakati wa mechi kati ya Utumishi na RAS Manyara katika viwanja vya Chuo Kikuu Dodoma.
Wachezaji wa timu ya mpira wa pete ya Utumishi na RAS Manyara wakifuata mpira wakati wa mechi iliyofanyika viwanja vya Chuo Kikuu Dodoma.
----
Timu ya mpira wa pete ya Utumishi imeanza vizuri mzunguko wa kwanza wa mashindano ya Shirikisho la Michezo ya Wizara na Idara za Serikali (SHIMIWI) baada ya kuifunga timu ya mpira wa pete ya Mkoa wa Manyara(RAS Manyara) mabao 36-8 katika viwanja vya Chuo Kikuu Dodoma(UDOM) leo mchana.
Katika mchezo huo, RAS Manyara ilianza kwa kasi kwa kumtumia mfungaji wake Maua Shabani (GS) aliyefunga mabao 3 kabla ya Utumishi kuanza kuumiliki mchezo huo kwa kutumia wafungaji wake Fatma Ahmed (GS) na Anna Msulwa (GA) walioshirikiana na hatimaye kuiwezesha Utumishi kuongoza kwa mabao 18-4 hadi kipindi cha kwanza kinamalizika.
Kipindi cha pili cha mchezo kiliongozwa na Timu ya Utumishi iliyoweza kuwatumia wachezaji wake mahiri Amina Ahmed (GD), Elizabeth Fusi (C),Monica Aloyce (GK) wakishirikiana na wafungaji wake na kuipatia Utumishi mabao 18-4 .Mpaka mchezo unamalizika Utumishi iliibuka mshindi kwa mabao 36-8 dhidi ya RAS Manyara.
Akiongea mara baada ya mchezo huo kocha wa timu ya mpira wa pete ya Utumishi Bw.Mathew Kambona alisema timu yake haikucheza katika kiwango kinachotakiwa kwa kuwa wapinzani walikuwa wanapewa nafasi ya kushambulia.
“Pamoja na kupata ushindi huu lakini timu yangu haikucheza katika kiwango kinachotakiwa hivyo inatakiwa ifanye juhudi zaidi kucheza katika kiwango cha juu” alisema Bw.Kambona.
Bw.Kambona aliongeza kuwa timu ya Utumishi ingepata mabao mengi zaidi lakini kutokana na makosa ya kiufundi maadui wamepata nafasi ya kuifunga timu hiyo.
Naye Katibu wa mpira wa pete wa RAS Manyara Bi.Flora Mollel alisema timu yake imeshindwa kuchukua ubingwa kutokana na uchovu wa safari.
Alisema,timu hiyo imejipanga vizuri kwa mashindano yajayo hivyo timu nyingine zitegemee maajabu ya RAS Manyara kuanzia leo.
Katika hatua nyingine timu ya Utumishi inatarajia kucheza na timu ya Wizara ya Ujenzi Jumatatu ya Septemba 22 mwaka huu.
Mechi kati ya Utumishi na RAS Manyara ni kati ya mechi zilizo kwenye mzunguko wa awali kabisa wa mashindano ya SHIMIWI wa kuchagua timu zitakazoingia robo fainali baada ya kupata washindi katika makundi tofauti tofauti.
Toa Maoni Yako:
0 comments: