Waziri mkuu wa Thailand Bi. Yingluck Shinawatra (kushoto) akiwasili
uwanja wa ndege wa Mwalimu Julius Nyerere akitokea katika hifadhi ya
Taifa ya Serengeti mkoani Mara akiwa ameambatana na mwenyeji wake Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Jakaya Kikwete (katikati) . Bi.
Shinawatra amemaliza ziara yake ya siku 3 nchini Tanzania.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Jakaya Kikwete akiwa na baadhi
ya viongozi wa jiji la Dar es salaam wakipunga mkono kumuaga rasmi
Waziri mkuu wa Thailand leo katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Mwl.
Julius Nyerere.
Rais Jakaya Kikwete akizungumza jambo na Waziri mkuu wa Thailand Bi.Yingluck Shinawatra katika uwanja wa kimataifa wa ndege wa Mwalimu Julius Nyerere leo jijini Dar es salaam.
Waziri mkuu wa Thailand Bi. Yingluck Shinawatra akiwapungia mkono kuwaaga baadhi ya wakazi wa jiji la Dar es salaam na viongozi wa Serikali wakiongozwa na Rais Jakaya Kikwete mara baada ya kukamilisha ziara yake ya siku 3 nchini Tanzania.
Picha na Aron Msigwa -MAELEZO.
Toa Maoni Yako:
0 comments: