Mshindi wa promosheni ya Tigo “Miliki Biashara Yako” Bw. Nicolaus Sanga (43) akijaribu Bajaji yake mpya yenye thamani ya Tsh 6,700,000 aliyokabidhiwa kutoka kwa Meneja Chapa wa Tigo Bw. William Mpinga anayeshuhudia.
 Meneja Chapa wa Tigo Bw. William Mpinga (katikati) akimkabidhi ufunguo wa Bajaji mmoja wa washindi wa promosheni “Miliki Biashara Yako” Bi. Isabella Msemo (24) katika hafla iliyofanyika Mbagala Zakhiem jijini Dar es Salaam. Anayeshuhudia kushoto ni Meneja Bidhaa wa Tigo Bw. Husni Seif.
 Mshindi wa Tigo “Miliki Biashara Yako” Bi. Evelyn Massawe (22) mkazi wa Dar es Salaam ambaye ni mwanafunzi wa chuo MAKUMIRA akipokea ufunguo wa Bajaji yake mpya yenye thamani ya Tsh 6,700,000 kutoka Meneja Chapa wa Tigo Bw. William Mpinga katika hafla iliyofanyika Mbagala Zakhiem jijini Dar es Salaam.
 Mshindi wa Tigo “Miliki Biashara Yako” Bw. Khalid Gomani (27) akikagua Bajaji yake mpya mara baada ya kukabidhiwa na Meneja Chapa wa Tigo Bw. William Mpinga (kushoto). Bajaji hizo zina warranti ya miezi 7.
 Washindi wa Tigo “Miliki Biashara Yako” wakipongezana mara baada ya kukabidhiwa Bajaji zao rasmi na Meneja Chapa wa Tigo Bw. William Mpinga (katikati). Tigo tayari imelipia leseni ya barabarani (road license) na bima kwa ajili ya Bajaji hizo.
Meneja Chapa wa Tigo Bw. William Mpinga katika mahojiano na Waandishi wa Habari. Kwanza aliwapongeza washindi wote 7 wa droo hii ya pili, pia alikumbushia kwamba kila mteja wa Tigo anao uwezo wa kujishindia Bajaji moja kila siku kwa muda wa siku 60 kwa kuongeza vocha ya Tsh 1,000 tu kwa siku. Ili kuhakikisha kuwa wateja wengi wanafurahia promosheni hii, mteja hahitaji kuweka vocha ya Tsh 1000 kwa mkupuo mmoja ili kushiriki, anaweza kuongeza salio kidogo kidogo hadi kufikisha kiasi cha Tsh 1000 kwa siku na kuweza kuingia kwenye droo. Bajaji 50 zimebaki kushindaniwa.
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: