Waziri mkuu wa Thailand Bi. Yingluck Shinawatra akiwasili nchini Tanzania kwa ziara ya siku tatu leo katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere jijini Dar es salaam.
Waziri mkuu wa Thailand Bi. Yingluck Shinawatra akikagua gwaride la
heshima la vikosi vya ulinzi na usalama vya Tanzania mara baada ya
kuwasili nchini Tanzania leo.
Gwaride la vikosi vya ulinzi na usalama vya Tanzania likipita mbele ya jukwaa kutoa heshima kwa Waziri mkuu wa Thailand Bi. Yingluck Shinawatra (kulia) na mwenyeji wake Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Jakaya Kikwete wakati wa mapokezi ya kiongozi huyo leo jijini Dar es salaam.
Waziri mkuu wa Thailand Bi. Yingluck Shinawatra akiangalia vikundi vya
ngoma akiwa na mwenyeji wake rais Jakaya Kikwete leo jijini Dar es
salaam.
Rais Jakaya Kikwete (kulia) akimkaribisha Ikulu jijini Dar es salaam waziri mkuu wa Thailand Bi. Yingluck Shinawatra (kushoto) mara baada ya kuwasili nchini Tanzania kwa ziara ya siku tatu.
Waziri mkuu wa Thailand Bi. Yingluck Shinawatra akiwa katika mkutano
wa pamoja na viongozi wa Tanzania Ikulu jijini Dar es salaam.
Naibu Waziri mkuu wa Thailand ambaye pia ni Waziri wa Mambo ya Nje wa
Thailand Dr. Surapong Tovichakchaikul (kushoto) na Waziri wa Fedha wa
Tanzania Mh. William Mgimwa (kulia) wakibadilishana hati za makubaliano
ya kudumisha , kutunza na kuendeleza uwekezaji kati ya Tanzania na
Thailand Ikulu jijini Dar es salaam.
Rais Jakaya Kikwete akizungumza wakati wa mkutano wa viongozi wa Tanzania na Thailand walioongozwa na Waziri mkuu wa nchi hiyo Bi. Yingluck Shinawatra ambapo Tanzania na Thailand zimesaini mikataba minne ya makubaliano ya kubadilishana wafungwa, uendelezaji wa shughuli za uwekezaji, ushirikiano katika masuala ya Ufundi na ushirikiano katika sekta ya Nishati na Madini.
Picha na Aron Msigwa – MAELEZO.
Toa Maoni Yako:
0 comments: