Naibu Waziri Angellah Jasmine Kairuki akizungumza katika hafla ya
uzinduzi rasmi wa huduma ya mpya ya kidijitali za Wakala wa Usajili
Ufilisi na Udhamini (RITA) ambazo zitawawezesha wananchi wote wenye simu
za mkononi na mtandano kupata huduma mbali mbali za RITA kwa kutumia
simu zao za mikononi.
Mkurugenzi Mtendaji wa Push Media Mobile, Freddie Manento akifafanua
jambo katika wakati wa uzinduzi wa huduma ya mpya ya kidijitali za
Wakala wa Usajili Ufilisi na Udhamini (RITA) ambazo zitawawezesha
wananchi wote wenye simu za mkononi na mtandano kupata huduma mbali
mbali za RITA kwa kutumia simu zao za mikononi. kulia ni Naibu Waziri
Angellah Jasmine Kairuki na kushoto ni Afisa Mtendaji Mkuu wa RITA,
Phillip Saliboko.
Naibu Waziri wa Katiba na Sheria, Angellah Kairuki akizindua tovuti ya RITA ambayo itawawezesha wananchi kupata huduma mbali mbali za Vizazi na Vifo.
---
Na Mwandishi wetu
NAIBU Waziri wa Katiba na Sheria, Mheshimiwa Angellah Kairuki amezindua huduma ya mpya ya kidijitali za Wakala wa Usajili Ufilisi na Udhamini (RITA) ambazo zitawawezesha wananchi wote wenye simu za mkononi na mtandano kupata huduma mbali mbali za RITA kwa kutumia simu zao za mikononi.
Katika huduma hiyo, wananchi wataweza kupata huduma zote zinazotolwa na RITA kwa kuchagua kipengele anachotaka baada ya kutuma neno RITA kwenda namba 15584 na kupokea muongozo utakaomwezesha kujua utaratibu wa kusajili kizazi au kifo kilichotokea hospitali na kwengine.
Pia wanaweza kupata taraifa zao mbali mali kwa kutembelea tovuti ya wakala hao, www.rita.go.tz, kwa kujiunga na mtandao wa kijamii wa www.facebook.com/ritatanzania na www.twitter.com/ritatanzania.
Toa Maoni Yako:
0 comments: