Mkurugenzi Mtendaji wa Kituo cha Uwekezaji nchini (TIC) Juliet Kairuki akizungumza na wageni waalikwa wakati wa uzinduzi rasmi wa Ripoti ya Uwekezaji ya Dunia ya Mwaka 2013 ambayo imejikita kiundani zaidi kuangalia muunganiko wa Mahusiano ya Kibiashara na Uwekezaji Duniani.
Bi. Kairuki amesema Tanzania imeweza kupata Uwekezaji mara dufu katika maeneo ya Mafuta na Utafiti wa Gesi Asilia katika kusukuma pato la taifa kuongeza ajira na kupambana na umaskini.
Ameongeza Muunganiko wa Biashara na uwekezaji umepata mwamko mkubwa sana kutoka kwenye makampuni makubwa duniani na umeleta fursa kwa nchi maskini na zinazoendelea kama Tanzania kuwa na uhusiano mzuri kiuchumi na nchi zilizoendelea. Uzinduzi huo umefanyika leo jijini Dar kwenye ukumbi wa mikutano wa Shirika la Kazi Duniani (ILO). Picha na Zainul Mzige.
Baadhi ya wageni waalikwa kutoka taasisi mbalimbali na mabalozi wakifuatilia uzinduzi rasmi wa ripoti hiyo ya Uwekezaji Duniani.
Mkuu wa Masuala ya Ufundi Ushirikiano na Huduma wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Maendeleo ya Biashara (UNCTAD) Manuela TORTORA akizungumzia umuhimu wa sera za nchi za Uwekezaji kuhakikisha zinatoa fursa ya ajira na kupunguza umaskini katika nchini zinazoendelea.
Viongozi wa taasisi mbalimbali, Mabalozi, Waandishi wa habari katika uzinduzi huo.
Mwezashaji katika uzinduzi wa Ripoti ya Ywekezaji wa Kigeni Duniani ya Mwaka 2013 Stella Vuzo Afisa Habari wa Kitengo cha Habari cha Umoja wa Mataifa (UNIC) akiwakaribisha Mkurugenzi Mtendaji wa Kituo cha Uwekezaji nchini (TIC) Juliet Kairuki na Mkuu wa Masuala ya Ufundi Ushirikiano na Huduma wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Maendeleo ya Biashara Manuela TORTORA kuzindua rasmi ripoti hiyo.
Mkurugenzi Mtendaji wa Kituo cha Uwekezaji nchini (TIC) Juliet Kairuki na Mkuu wa Masuala ya Ufundi Ushirikiano na Huduma wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Maendeleo ya Biashara Manuela TORTORA kwa pamoja wakizindua rasmi Ripoti ya Uwekezaji Duniani ya Mwaka 2013 iliyobeba kauli mbiu Muunganiko wa Biashara na Uwekezaji Duniani "Global Value Chains".
Sasa imezinduliwa rasmi nchini Tanzania.
Mwakilishi wa Shirika la Umoja wa Mataifa la kuendeleza Viwanda (UNIDO) Emmanuel Kalenzi akichangia mada baada ya uzinduzi wa Ripoti ya Uwekezaji Duniani ya Mwaka 2013.
Kutoka kushoto Meza kuu ni Mkurugenzi wa Utafiti na Mifumo ya Teknolojia kutoka Kituo cha Uwekezaji nchini (TIC) John Kyaruzi, Mkurugenzi Mtendaji wa Kituo cha Uwekezaji nchini (TIC) Juliet Kairuki na Mkuu wa Masuala ya Ufundi Ushirikiano na Huduma wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Maendeleo ya Biashara (UNCTAD) Manuela TORTORA.
Usia Nkhoma Ledama kutoka Kitengo cha habari cha Umoja wa Mataifa (UNIC) akigawa Ripoti ya Uwekezaji Duniani ya Mwaka 2013 kwa wadau waliohudhuria uzinduzi wa ripoti hiyo.
Mdau akipitia ripoti hiyo mara baada ya kuzinduliwa rasmi nchini.
Pichani juu na chini ni sehemu ya wageni waalikwa waliohudhuria uzinduzi huo.
Toa Maoni Yako:
0 comments: