NA CHRIS MAUKI
1. Usipende kuamka mapema, endelea kujigeuza geuza na kupiga miayo kitandani, kwani kama hakuna papasi au viroboto, una haraka gani kuwahi kuamka?

2. Usipangilie namna ya kutumia fedha zako. Upatapo fedha tu, we zitumie hapo hapo na zikiisha wala usifikirie jinsi ulivyozitumia. Kesho itajijua yenyewe.

3. Usiwaze mambo ya kuhifahi fedha benki, subiri hadi uwe na mamilioni, kwanza uta ‘save’ vipi wakati unamahitaji mengi? Hao wanaokushauri uweke fedha benki hawakuonei huruma na mahitaji yako.

4. Kamwe usijishuhulishe katika zile shuhuli nyingine ambazo unaziita za wasioenda shule. Yani we msomi wa chuo kikuu unafanya biashara ndogo ndongo au kuwa na mifugo au shamba? Hizo ni kwa wale wasiojua shule.

5. Usifikirie kuanzisha biashara hadi malaika atoke mbinguni akuletee mtaji. Kwanza utaweza vipi wakati huna mamilioni? Kwanza wewe hauko ‘level’ moja na hao wanaoanzisha vibiashara vya hela ndogo. We ni wa muhimu sana.

6. Laumu kila kitu, laumu serikali, laumu mabenki, kwa kutokukopesha fedha, laumu saccos pia kwa kuwa fedha zinazowekwa huko zaweza kuibiwa au kuliwa. Laumu bosi au mwajiri wako kwa kutokupa mshahara mkubwa wa kuweza kuwekeza.

7. Tumia zaidi ya mapato yako ili kulifanikisha jambo hili, nunua zaidi vitu vya matumizi kwa mkopo, na azima fedha kwa marafiki na ikiwezekana mkope hata mwajiri (si utakatwa kidogo kidogo kwenye mshahara?), kama mwajiri hataki kukukopa, basi mwombe mshahara wa awali (advance salary) ili uweze kujinunulia unachotaka kama vile simu ya bei ghali, macheni, mapete, mahereni ya dhahabu n.k. Maisha yenyewe mafupi inabidi ujifurahishe.

8. Fanya ushindani na mavazi ya bei kubwa, hakikisha unavaa nguo zilizo katika chati kuliko wafanyakazi wenzako au rafiki zako wote. Wakati wowote jirani au rafiki yako anaponunua simu wewe nenda kanunue ya gharama zaidi yake ili umkomeshe akuheshimu.

9. Jinunulie gari zuri na la kifahari ambalo linagharimu mara tatu ya mshahara wako wa mwaka mzima. Hii itakusaidia kukuweka muda mrefu ukilipa deni la gari na sio shuhuli nyingine za maendeleo.

10. wape watoto wako kila kitu wanachohitaji, kwa sababu wewe ni mzazi mzuri unayejali, usiwaache wahangaike kupata chochote wakati wewe upo hai kwa ajili yao mtoto hakui kwa mzazi bwana! Kwa hali hii watafanikiwa kukua wakiwa wazembe, wavivu na hivyo kuwa masikini kiasi ambacho hawataweza kukujali katika uzee wako. UKIFUATA HIZI KANUNI LAZIMA UTAFANIKIWA KUUKARIBISHA UMASKINI ULIO THABITI NYUMBANI KWAKO.
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

1 comments:

  1. HIIPOST ITAKUWA NZURI ZAIDI KAMA ITAGEUZWA NA KUWA NA UHALISIA WAKE KAMILI LAKINI IKIBAKIA HIVI WATAKAOIELEWA NI WA`CHACHE.BUT OTHERWISE IT IS A VERY AWASOME POST I LIKED IT

    ReplyDelete