Hatima ya msanii anayeshiriki katika video za wasanii wa muziki wa bongo fleva, Agnes Jerald 'Masogange' na mwenzake Melisa Edward, waliokamatwa nchini Afrika Kusini na dawa za kulevya kesi yao inatarajiwa kusomwa tena tarehe 13 Agosti mwaka huu nchini humo.
Akizungumza jijini Dar es Salaam, Kamanda wa Polisi wa Kikosi cha Kudhibiti Dawa za Kulevya Tanzania, Godfrey Nzowa aliweka wazi kuwa wanadada hao wawili tayari walishapandishwa kizimbani wiki iliyopita.
Aidha alisema kuwa kutokana na ushahidi kutokukamilika ndiyo sababu ya akinadada hao kusubiri kupanda kizimbani tena tarehe 13 ya mwezi ujao.
Toa Maoni Yako:
0 comments: