07/01/2013 - 08/01/2013
Kila Mwanaume anatamani Mwanamke mzuri, Mrembo, na mwenye mafanikio ili asiwe Kaseja wa nyumba yako... Lakini, Umewahi kujiuliza swali huyo Mwanamke amefikaje hapo?? Hudhani kuna Mwanaume mwenzio aliyemkubali from Scratch, akajitoa, akampamba, wengine wametoa mishahara yao wamesomesha,mtoto wa watu amenawiri inye ndembendembe uso unang'aa,we unakumbana nae kitaani unataka kuunga tela tu kiulaini...Blaza sio rahisi kiivyo, tafuta wako andunje umpambe na wewe mpaka afikie hadhi ya kutamaniwa na wengine uone inavyouma.

...Na wewe Mwanamke unayetamani Mwanaume mzuri, anayejua kuvaa,na mwenye mafanikio,gari nzuri na kazi nzuri... Unadhani amefika hapo by Photosynthesis na Osmosis process??? 

Kuna mtu amesacrifice maisha yake kumshape huyo mwanaume... amekuja mjini anavaa suruali ya kitambaa na Sandles.. akamfundisha kuna Pierre Cardin..Amekuja na kikwapa cha njano akafundishwa kutumia Deodorant na kununua Isa Miyake, wewe unakumbana nae ananukia, yuko kwenye gari nzuri, unaanza kumtega-tega na vipedo vyako vya Pink na kumuachia mapaja na maziwa nje. Kirahisi tu!..

Uwe na huruma na nguvu za watu wewe Guberi upendaye mteremko...

Ukitaka kizuri tengeneza chako ili ukifaidi kikishapendeza na sio Kudandia Mafanikio ya wenzio waliochumia juani halafu wewe unaandaa Kivuli tu, wenzio wahangaike weeee ili wewe uje kucheza bila kukunja goti...

Imetolewa na;
Mkuu wa Chuo cha Mapenzi
Seth Giovanni
Moja ya usafiri maarufu unaotumiwa na wakazi wa mji wa Shinyanga ni Baiskeli ambazo wao wamezigeuza kuwa ni kitega uchumi chao kwa kufanya shughuli za usafirishaji wa abiria (daladala). Pichani wanaoneka vijana wakisubiri abiria.
Waziri mkuu wa Thailand Bi. Yingluck Shinawatra akiwasili nchini Tanzania kwa ziara ya siku tatu leo katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere jijini Dar es salaam.
 Waziri mkuu wa Thailand Bi. Yingluck Shinawatra akikagua gwaride la heshima la vikosi vya ulinzi na usalama vya Tanzania mara baada ya kuwasili nchini Tanzania leo.
Gwaride la vikosi vya ulinzi na usalama vya Tanzania likipita mbele ya jukwaa kutoa heshima kwa Waziri mkuu wa Thailand Bi. Yingluck Shinawatra (kulia) na mwenyeji wake Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Jakaya Kikwete wakati wa mapokezi ya kiongozi huyo leo jijini Dar es salaam.
  Waziri mkuu wa Thailand Bi. Yingluck Shinawatra akiangalia vikundi vya ngoma akiwa na mwenyeji wake rais Jakaya Kikwete leo jijini Dar es salaam.
Rais Jakaya Kikwete (kulia) akimkaribisha Ikulu jijini Dar es salaam waziri mkuu wa Thailand Bi. Yingluck Shinawatra (kushoto) mara baada ya kuwasili nchini Tanzania kwa ziara ya siku tatu.
 Waziri mkuu wa Thailand Bi. Yingluck Shinawatra akiwa katika mkutano wa pamoja na viongozi wa Tanzania Ikulu jijini Dar es salaam.
 Naibu Waziri mkuu wa Thailand ambaye pia ni Waziri wa Mambo ya Nje wa Thailand Dr. Surapong Tovichakchaikul (kushoto) na Waziri wa Fedha wa Tanzania Mh. William Mgimwa (kulia) wakibadilishana hati za makubaliano ya kudumisha , kutunza na kuendeleza uwekezaji kati ya Tanzania na Thailand Ikulu jijini Dar es salaam.
Rais Jakaya Kikwete akizungumza wakati wa mkutano wa viongozi wa Tanzania na Thailand walioongozwa na Waziri mkuu wa nchi hiyo Bi. Yingluck Shinawatra ambapo Tanzania na Thailand zimesaini mikataba minne ya makubaliano ya kubadilishana wafungwa, uendelezaji wa shughuli za uwekezaji, ushirikiano katika masuala ya Ufundi na ushirikiano katika sekta ya Nishati na Madini.

Picha na Aron Msigwa – MAELEZO.
Mkurugenzi Mkuu wa Zantel, Pratap Ghose akizungumza na wafanyakazi wakati wa Futari.JPG
Mkurugenzi wa Zantel, Pratpa Ghose akiongozana na Afisa Rasirimali watu, Francis Kiaga.

Wafanyakazi wa Zantel wakichukua chakula.

Wafanyakazi wa Zantel wakijumuika kupata futari.
---
Kampuni ya simu za mikononi ya Zantel jana iliwaandalia wafanyakazi wake futari katika makao makuu ya kampuni hiyo ikiwa ni sehemu ya kuimarisha mahusiano baina ya wafanyakazi katika msimu huu wa mfungo wa Ramadhan.

Akizungumza na wafanyakazi hao wakati wa hafla hiyo Ofisa Mtendaji Mkuu wa Zantel, Bwana Pratap Ghose aliwataka wafanyakazi hao kuimarisha urafiki na upendo kati yao.

Alisema kuwa katika kipindi hiki cha mfungo wafanyakazi wakiwa kama waumini wengine wa dini ni vema wakatambua kuwa kipindi hiki cha mfungo ni kipindi cha kukaa pamoja na kutafakari mazuri ambayo wanatakiwa kuyafanya kati yao pamoja na jamii nzima inayowazunguka.

“Hiki ni kipindi muhimu sana kwetu wafanyakazi wote kwa ujumla katika kujitafakari kwa kiasi gani tumeishi katika jamii zetu na wenyewe kwa ujumla huku tukijiimarisha zaidi katika imani zetu za kidini” alisema Pratap.

Katika hafla hiyo wafanyakazi hao walipata wasaha wa kuulizana maswali yahusuyo utendaji wa kazi zao pamoja na maswali mengine ya chemsha bongo.
IMG_1336
Mstahiki Meya wa Manispaa ya Ilala Jerry Silaa akizungumza na uongozi wa Al Madrassatul Munauwaratul Islamiya iliyopo Msasani Bonde la Mpunga Ofisini kwake leo jijini Dar es Salaam wakati wa hafla fupi ya kukabidhi Spika mbili, Vipaza sauti viwili (Microphones) pamoja na Amplifaya ambavyo vitatumika kuendeshea shughuli mbalimbali za kueneza mafunzo ya dini kwa jamii na watoto wanaosoma chuoni hapo. Vifaa hivyo vimetolewa na mdau mpenda maendeleo kupitia kwa Mstahiki Meya wa Manispaa ya Ilala Jerry Silaa.
IMG_1345
Pichani juu na chini ni Mstahiki Meya wa Manispaa ya Ilala Jerry Silaa pamoja na Bw. Abdulmalik Ibrahim (kulia) aliyemwakilishi mdau aliyetoa vifaa hivyo (jina kapuni) wakikabidhi Spika tatu, vipaza sauti viwili na Mixer kwa Katibu wa Madrasa hiyo Bw. Salim Amri (wa pili kushoto) aliyeambatana na Ustaadh Nurdin Nassor Abdallah (katikati). Kushoto ni mmoja wa walimu wa madrassatul Munauwaratul Islamiya kilichopo Msasani Bonde la Mpunga Ustaadh Mohamed Kassim.
IMG_1339
IMG_1344
Mstahiki Meya Jerry Silaa akikagua moja vifaa hivyo alivyokabidhi leo ofisini kwake .
IMG_1360
Ustaadh Nurdin Nassor Abdallah wa Al Madrassatul Munauwaratul Islamiya ya Msasani Bonde la Mpunga akitoa shukrani kwa Mstahiki Meya Jerry Silaa pamoja na mdau alijitolea baada ya kupokea vifaa hivyo ambavyo amesema vitawasaidia katika kazi zao za kueneza neno la Mungu hasa kipindi hichi cha mfungo wa mwezi mtukufu wa Ramadhani ikiwemo kuhubiri Amani nchini.
IMG_1372
Uongozi wa Al Madrassatul Munauwaratul Islamiya kilichopo Msasani Bonde la Mpunga wakiomba dua za baraka kwa msaada waliopokea leo ofisini kwa Mstahiki Meya Jerry Silaa.
Mkurugenzi Mtendaji wa Airtel Tanzania, Sunil Colaso (wa pili kushoto) akiwakaribisha baadhi ya wateja wao katika hafla ya futari iliyoandaliwa na kampuni hiyo jijini Dar es Salaam jana. Kushoto ni Mkurugenzi wa Mawasiliano wa Airtel, Beatrice Singano Mallya.
Mkurugenzi Mtendaji wa Airtel Tanzania, Sunil Colaso (kushoto)
akimkaribisha Ofisa Mkuu wa Fedha wa Benki ya NMB, Waziri Barnabas
katika hafla ya futari iliyoandaliwa na Airtel kwa wateja wao jijini
Dar es Salaam jana.
Baadhi ya wateja wa kampuni ya simu za mkononi ya Airtel Tanzania
wakichukua mlo wa futari iliyoandaliwa na kampuni hiyo jijini Dar es
Salaamu juzi.
Wateja wa Airtel Tanzania wakichukua mlo wa futari iliyoandaliwa
na kampuni hiyo jijini Dar se Salaam juzi.
Mhariri Mtendaji Mkuu wa Mwananchi Communications, Bakari Machumu
(wa pili kulia) na Mkurugenzi Mtendaji wa Airtel Tanzania, Sunil
Kolaso (kulia kwake) wakichukua mlo wa futari iliyoandaliwa na Airtel
kwa wateja wake jijini Dar es Salaam juzi.
Mkurugenzi wa Kampuni ya Azam, Said Salim Bakhresa (wa pili kushoto), akichukua mlo wa futari pamoja na baadhi ya wateja wa Airtel katika hafla iliyoandaliwa na kampuni hiyo kwa wateja wake jijini Dar es Salaam juzi.
Baadhi ya wateja wa kampuni ya simu za mkononi ya Airtel Tanzania wakifuturu katika hafla iiliyoandaliwa na kampuni hiyo jijini Dar es Salaamu juzi.
Showlove...
Wasichana hawa ni mapacha ambao walijitokeza kwenye usaili wa shindano la Epiq Bongo Star Search (EBSS) uliofanyika kwenye uwanja wa taifa Dar es salaam, walilazimika kuimba pamoja na ni tukio la kwanza kwa washiriki wawili kuimba pamoja kwenye usaili
Umati wa vijana uliojitokeza kwenye usaili wa EBSS 2013 kwenye uwanja wa taifa jijini Dar.
Wasichana hawa mapacha waliojitokeza kwenye ushiriki wa shindano la EBSS 2013 mkoani Dar es salaam akisikiliza jambo kutoka kwa Jaji Mkuu wa EBSS Ritha Paulsen.Shindano la kuimba la Epiq BSS limemaliza usaili wake ambao kwa mwaka huu umefanyika katika mikoa sita ya Arusha, Mbeya, Mwanza, Zanzibar, Dodoma na kumalizia Dar es Salaam.
Umati wa vijana uliojitokeza kwenye usaili wa EBSS 2013 kwenye uwanja wa taifa
Mwanafunzi wa kidato cha nne katika sejkondari ya Yusuph Makamba, Dar es salaam akifurahi baada ya kupita awamu ya kwanza ya shindano la EBBS 2013.
Usaili wa Dar es Salaam uliofanyika mwishoni mwa wiki hii ndio umehitimisha zoezi la kusaka vipaji, huku mwishoni mwa wiki hii washiriki wakijiandaa kuingia kambini kwa ajili ya mchujo wa kwanza.

Wiki hii washiriki waliopatikana mikoani wataungana na washiriki wa hapa Dar es salaam katika mchujo wa awali wa kupata washiriki watakaoingia katika kambi rasmi ya EBSS 2013.

Kwa mkoa wa Dar es salaam washiriki waliopatikana ni 20 huku mikoa mingine ya Arusha, Mwanza, Dodoma, Mbeya na Zanzibar washiriki waliopatikana ni sita kila mkoa hivyo kufanya jumla wa washiriki watakaoingia katika mchujo wa awali kuwa 50.

Shindano hilo ambalo mwaka huu lilikuwa na utaratibu mpya wa kutumia majaji wenyeji kutoka katika kila mkoa, ambapo kwa upande wa Mbeya kulikuwa na majaji ambao ni watangazaji wa radio huku usaili wa Dar es Salaam ukichagizwa na mchezaji wa mchezo wa mpira wa kikapu wa ligi ya Marekani (NBA) Hashim Thabeet aliyekuwa kama jaji mwalikwa.

Akizungumza na baadhi ya wahiriki waliojitokeza Hashim aliwataka vijana kutokata tamaa katika kutafuta mafanikio kupitia muziki.

Alisema kuwa anaamini Tanzania kuna vipaji vingi vya muziki ambavyo vinatakiwa kuendelezwa kufikia viwnago vya kimataifa, lakini ili kufanikisha hilo inatakiwa vijana wenyewe kujiamini na kuongeza nia ya kweli katika kutafuta kung’arisha nyota zao.

Aliwataka kutambua kuwa nidhamu na kujituma ndio siri kubwa ya mafanikio katika sanaa na kazi yoyote ile na hivyo aliwasihi kujitambua na kutafuta mfanikio hayo.

Akizungumzia shindano hilo kwa mwaka huu, jaji mkuu wa shindano hilo, Ritha Paulsen alisema mchuano utakuwa mkali hasa kutokana na kuchagua washiriki wakali kutoka kila mkoa.

‘Mwaka huu ushindani utakua mkali kuliko mwaka jana, lakini pia kutakuwa na burudani zaidi kutoka kwa washiriki kama ambavyo imezoeleka’ alisema Ritha.

Naye Afsa Biashara Mkuu wa Zantel, Sajid Khan alisema Zantel imezidi kuboresha shindano hilo, huku akiwataka watanzania watarajie makubwa zaidi mwaka huu katika kuzalisha vipaji na pia kupata burudani kubwa.

‘Tutatoa zawadi kadha wa kadha shindano litakapoanza, lakini pia wale ambao bado wanataka kushriki wanaweza kutumia njia ya simu kufanya usaili wao’ alisisitiza Khan.

Washiriki wanaotaka kufanya usaili kwa njia ya simu wanapaswa kupiga namba 0901551000 au watume ujumbe mfupi kwenda 15530 kupata maelezo ya namna ya kujiunga.

Naitwa Mathew Yinza Telles.Nimezaliwa tarehe 08 July 1992.Jina langu la sanaa naitwa Yincas El Legendee Nickname Killerflo.Jina la Yincas limetokana na jina langu la Yinza ambalo idadi kadahaa ya watu wananifahamu kwa jina hilo.Ukiachana na mzik,pia ni mwanafunzi wa chuo kikuu Mzumbe kilichopo Morogoro nachukua Stashahada ya kwanza ya Health Systems Management.Nimemaliza kidato cha nne katika shule ya St. Francis De Sales na kujiunga na shule ya Loyola High School ambapo nilihitimu kidato cha sita na kufanikiwa kufaulu vizuri kwenda chuo kikuu Mzumbe.Katika familia yangu mimi ni mtoto wa pili nikitanguliwa na dada yangu na mdogo wangu wa kike wa mwisho.Napenda sana mpira wa miguu ni mchezaji mzuri na shabiki wa Arsenal FC,pia napenda sana kuskiliza mziki wa dunia nzima kuanzia hapa nyumbani Tanzania na nchi zingine zote duniani.Napenda sana mziki wa HipHop na ni shabiki wa Rapper wa kimarekani anaeitwa Fabolous ’Loso’ na hapa nyumbani namkubali Fid Q na Ngwea..R.I.P bro.

Safari yangu ya mziki nimeanza mwaka 2007 ndipo nilirecord traki ya kwanza iliyoitwa ‘Ishara Ya Ukombozi’ nilikuwa nipo kidato cha pili na nilimshirikisha kaka yangu wa shule aliitwa ‘Culture’ ambae aliniandikia mistari na produza alikua Dizzy Mchizy.Baada ya hapo nikarekodi trak nyingine iliyoitwa ‘Modern Crunk’ na kuifanyia video iliyopata airtime katika baadhi ya station ikiwemo C2C.Pia sikuishia hapo,mwaka 2008 nikarekodi nyimbo nyingine iliyoitwa ‘Niache Niongee’ chini ya produza Dizzy Mchizy ambayo kwa namna moja au nyingine ilifanya watu waanze kunielewa kwamba nina kipaji.Baada ya kufaulu na kuingia kidato cha tano ndipo nikakutana na Dully Sykes na kufanya nae nyimbo pale Dhahabu Records iliyoitwa BELIEVE ME mwaka 2010 lakin bahati mbaya nyimbo haikusogea kutokana na vikwazo mbalimbali ikiwemo shule kunibana.Mwaka huohuo nikapata idea ya kufanya mixtape yangu iliyoitwa EL LEGENDEE 1 ambayo ilikua na nyimbo kama Believe Me,Niache Niongee,Love You,Don’t Go nk.Namshukuru Mungu mixtape watu waliipenda na kunipa moyo wa kukaza zaidi.Mwaka 2011-2012 ilikuwa ngumu kwa mi kufanya mzik kutokana na shule kunibana nilikuwa form6 ila nlifanya nymbo ya ‘Sweetlove’ na kuiweka mtandaoni ambayo ilipata downloads zaidi ya elfu3.Baada ya kumaliza form6 nilifanya video ya nyimbo ‘Imma Getting Em Off’ ambayo ilitazamwa sana YouTube na kupata sana airtime kwa baadhi ya Station hapa nchini.

Kwa sasa nina project ya kufanya Album Yangu itayoitwa ‘The Rise Of The Young Legendee’ na nishafanya baadhi ya nyimbo ambazo pia zipo kama Trailer katika mitandao mfano HulkShare/yincaskillerflo.Baadhi ya nyimbo hizo ni kama Sweetlove,Mr A Mill Swag,Show Me.Pia nimetoa Tshirts za kusapoti hii album ambazo zipo mtaani.Kwa sasa naachia video mbili za nyimbo zangu SATURDAY na R.I.P.Safari hii nimejipanga vilivyo,am ready for the competition,,you gotta get stay ready,,watu wangu wasubiri new flavour kwa industry.Nitakuwa mchoyo wa fadhila nisipowashukuru hawa watu,,Familia yangu inayonisapoti,Dizzy Produza, Yuddy, Dully Sykes na wanangu wa RoyalFAM(makaino, caliross, jose, sonjay, na mtu mzima BigDadi Kimambo) Na watu wangu wote wanaonisapoti mziki wangu kwa namna moja au nyingine... Nawapenda sana. Follow Me SoundCloud/yincaskillerflo... Instagram/yincaskillerflo... HulkShare/yincaskillerflo... YouTube/yincas08… AHSANTE

#Its Western Musik SwagginUp_RoyalF

EMBED CODE TO MY VIDEO TEASER :
 Kuni zinauzwa kuanzia shilingi mia tano kwa fungu...
 Mama Lishe nao wapo japo mazingira yao hayaridhishi kwa afya ya walaji.
 Mtaro wa maji taka nao unakatiza katikati ya soko...
Hali ya usafi halidhishi kabisa maana wengi wamekuwa wakipanga bidhaa zao maeneo ambao si salama kwa afya.
 Meneja chapa wa Tigo Bw.William Mpinga akiongea na waandishi wa habari hawapo pichani wakati wa kuchezesha droo ya pili ya bahati nasibu ya "Miliki Biashara Yako" ibuka na Bajaji, jumla ya washindi saba walipatikana ambao ni wa siku ya Jumatatu hadi Jumapili wiki iliyopita. Wengine pembeni ni Meneja wa Bidhaa wa Tigo Bw. Husni Seif na Mkaguzi toka bodi ya bahati nasibu ya taifa Bw. Bakari Maggid.
Meneja wa Bidhaa wa kampuni ya Tigo Bw. Husni Seif akibofya kompyuta kuchezesha droo ya "Miliki Biashara Yako" ibuka na Bajaji wakati wa mkutano na waandishi wa habari, wengine pichani ni Meneja Chapa wa Tigo Bw. William Mpinga na Bw. Bakari Maggid kutoka bodi ya bahati nasibu ya Taifa. Washindi hao watakabidhiwa Bajaji zao kesho pale Mbagala Zakhiem, Dsm.
Meneja chapa wa Tigo Bw.William Mpinga akiongea na moja ya washindi wa promosheni ya "Miliki Biashara Yako." Washindi waliopatikana ni Nicolus Maliyatabu Sanga (43) - mkazi wa Dsm, Julius Dilikwije - mkazi wa Same, Isabellah Edward Msemo (24) - Dsm, Eliasa Hamisi Mbano (48) - Tabora, Charles benedect Kato (41) - Kinyerezi, Evelyn Elisalia Massawe - (22) Mwanafunzi wa Chuo, mkazi wa Kimara, Khalidi Jafary Gomani (27) wa Dsm.