KEKI inayoonyesha maadhimisho ya Mwaka mmoja wa kipindi cha 'The Mboni Show' cha mwanadada Mboni Masimba ambaye ndiye muandaaji na msimamizi wa kipindi kinachorushwa na East Africa Television (EATV). Mwanadada huyo alitoa msaada wa vifaa vya hospitali hiyo ikiwa pamoja na kupaka rangi wodi ya wazazi na watoto. Jumla ya msaada wote aliotoa ulikuwa na gharama ya mil.5.
Meya wa Manispaa ya Ilala, Jerry Slaa akiongea machache wakati wa maadhimisho ya mwaka mmoja wa Kipindi cha The Mboni Show, Meya huyo aliwaasa vijana kufanya kazi kwa bidii na kujitoa kusaidia jamii. Pembeni yake ni Mganga Mkuu wa Hospitali ya Amana iliyopo manispaa ya Ilala.
 Meya wa Manispaa ya Ilala, Jerry Slaa akitia msisitizo wa jambo.
 Anayeongoza jahazi la kukata keki ni mwanadada Mboni Masimba msimamizi wa kipindi cha 'The Mboni Show' (katikati) akiwa pamoja na Meya wa manispaa ya Ilala, Jerry Slaa, Mganga Mkuu wa hospitali ya Amana, Mama mzazi wa Mboni pamoja na mdogo wake.
 Keki ikikatwa.
 Ndugu, jamaa, marafiki na wafanyakazi wa The Mboni Show pamoja na Wafanyakazi wa EATV waliungana kwa pamoja.
 Msanii Mad Ice akiimba...
 Mganga Mkuu akimpongeza Msanii Mad Ice mara baada ya kumkuna kwa wimbo wake.
 Msanii Mwasiti nae alitoa burudani kidogo.

Msaada wa Vifaa vilivyotolewa na Mwanadada Mboni Masimba kupitia kipindi chake cha 'The Mboni Show'
 Mafundi wakichanganya rangi kabla ya kuanza kupakwa.
 Zoezi la kupaka rangi likiendelea kwa watu wote waliohudhuria kumuunga mkono mwanadada Mboni Masimba.
 Wasanii Mad Ice na Mwasiti wakiwa na Mboni Masimba.
 Mwanadada Marygrory toka EATV ambaye ni msomaji mkuu wa Kajunason Blog nae aliungana na mwanadada Mboni Masimba kupaka rangi.
 Nikishow love na mwanadada Marygrory ambaye ni msomaji wangu mkuu.
 Nikishow Love na Mwanadada Mboni Masimba na Marygrory.
 Akifurahia na marafiki na wapenzi wa kipindi chake.
  Mwanadada Mboni Masimba akiwa na Swebe.
 Marafiki wakifurahia kwa pamoja.
 Furaha zilitanda mara baada ya zoezi la kupaka rangi kumalizika.
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: