Baada rais Barack Obama kutangaza kutembelea nchi 3 barani Afrika, bila kutembelea nchi yake ya asili ya Kenya, sasa Wakenya wahoji na kuona kuwa rais huyo ni msaliti.

Wakizungumza kwa nyakati tofauti na Kajunason Blog, wakenya hao walisema kuwa wanasikitishwa na kitendo cha rais huyo kuitembelea nchi ya Tanzania na kuiacha nchi yao ya Kenya.

"Tunasikitishwa sana na rais huyu wa Marekani Barack Obama kutembelea nchi ya Tanzania na kuiacha nchi yetu, maana wakenya wanahamu nae tokea ameingia madarakani ila amekuwa kimya hata kuja kuwasalimia licha ya kumtumia salamu za pongezi rais wetu Uhuru Kenyatta," Walilalama Wakenya hao.

Kuanzia tarehe 26 Juni hadi 3 Julai, Rais Obama na Mkewe wanatarajia kutembelea nchi za Senegal, Afrika ya Kusini na Tanzania. Katika ziara yake hiyo, Rais atawekea mkazo umuhimu ambao Marekani inauweka katika ushirikiano wetu wa kina na unaoendelea kuimarika na nchi za Afrika Kusini mwa Jangwa la Sahara kupitia mipango mbalimbali ikiwemo ile ya kuimarisha ukuaji wa uchumi, uwekezaji na biashara, uimarishaji wa taasisi za kidemokrasia na uwekezaji katika kizazi kipya cha viongozi wa Kiafrika.

Rais atakutana na viongozi mbalimbali wa kiserikali, sekta binafsi na jumuiya huru ya kiraia ikiwemo vijana ili kujadili ubia wetu wa kimkakati katika ushirikano wetu rasmi na masuala mengine ya kimataifa. Ziara hii itadhihirisha dhamira ya dhati ya Rais ya kupanua na kuimarisha ushirikiano kati ya Marekani na watu wa nchi za Afrika Kusini mwa Jangwa la Sahara katika kuimarisha amani na ustawi katika kanda hii na duniani kote kwa ujumla.
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: