Mkurugenzi wa Kampuni ya Intellectuals ambao ndiyo waandaaji wa mbio hizo, Innocent Melleck akiongea katika mkutano na waandishi wa habari wakati wa ufunguzi wa wadhamini wa Uhuru Marathon iliyofanyika leo jijini Dar es Salaam. Kushoto ni Katibu mkuu wa Chama Cha Riadha Tanzania, Seleman Nyambui.
Kampuni ya Intellectuals Limited, ambao ndio waasisi na waratibu wa mbio za Uhuru zijulikanazo kama “Uhuru Marathon” leo wametangaza kufungua rasmi milango kwa makampuni, mashirika na taasisi mbalimbali zitakazopenda kudhamini mbio hizi za aina yake nchini zitakazokuwa zikifanyika kila mwezi Desemba zikiambatana na maadhimisho ya sherehe za Uhuru wa Tanzania.

Akizungumza na waandishi wa Habari jijini Dar es salaam, mkurugenzi mkuu wa Intellectuals Ltd Bw. Innocent Melleck, alisema; Nadhani wote mnakumbuka uzinduzi wa mbio hizi za Uhuru, uliofanyika mwezi Desemba mwaka Jana, ukiwa unaashiria kuanza kwa mchakato wa maandalizi ya mbio zenyewe ambazo zitaanza kufanyika mwezi desemba mwaka huu 2013.
Katibu mkuu wa Chama Cha Riadha Tanzania, Seleman Nyambui, akizungumza na waandishi wa habari wakati wa ufunguzi wa wadhamini wa Uhuru Marathon iliyofanyika leo jijini Dar es Salaam. Kulia ni Mkurugenzi wa Kampuni ya Intellectuals ambao ndiyo waandaaji wa mbio hizo, Innocent Melleck.
Mbio hizi za Uhuru, kama lilivyo jina lake ni mbio zilizoanzishwa ili kuongeza chachu za watanzania kuwa na moyo wa kulinda Amani, Umoja na Mshikamano wetu, wakati tunaposherehekea sikikuu za Uhuru wa Taifa letu. Tangu tulipofanya uzinduzi mwezi desemba mwaka jana, sisi waratibu na viongozi wa chama cha riadha Tanzania (RT), tulianza mchakato wa maandalizi ya awali ya kufanikisha mbio hizi, ikihusisha kupanga mzunguko utakaotumika kwa mbio hizo n.k.

Kwa sasa maandalizi ya awali yanaendelea vizuri, nasi tumeona kuwa huu ni muda muafaka kufungua milango ya Udhamini kwa makampuni, mashirika na Taasisi mbalimbali ambazo zitahitaji kushirikiana nasi katika kufanikisha mbio hizi wajitokeze na kupata taratibu za udhamini. Tuna imani kubwa kuwa wapo wadau wengi wenye lengo la kufanikisha ajenda hii muhimu ya kuenzi Amani, Umoja na mshikamano wa Taifa letu. Mbio hizi zina vipengele vikuu vitatu;
i. Mbio Ndefu (Full Marathon 42 km)
ii. Mbio za Kati (Half Marathon 21 km) na
iii. Mbio za kujifurahisha (Fun run 5km)
Mdhamini atakayedhamini mbio ndefu (full marathon), ndie atakaebeba jina la Mashindano haya. Hivyo nawasihi wale wote wenye nia ya kudhamini kuanza kujitokeza sasa na kuchagua mbio zipi wanataka kudhamini ili taratibu nyingine zifuatie. Alisema Innocent.
Akizungumzia kuhusu upande wa ufundi, Katibu mkuu wa chama cha Riadha Taifa Bw. Suleyman Nyambui alisema; kwa upande wetu sisi RT, maandalizi ya awali yameshaanza kufanyika ikiwemo kupendekeza mzunguko wa mbio hizo na kuangalia mambo yote ya kiufundi yanayohusiana na mbio hizi.
Tunawaomba wadhamini wajitokeze ili kwa pamoja tuweze kufanikisha mbio hizi zenye malengo mazuri kwa Taifa letu kwa ujumla. Mbio hizi tutazisimamia na kuziendesha katika hadhi ya kimataifa ili kuhakikisha kuwa zaidi ya kulinda Amani na Umoja wetu, pia tunalitangaza Taifa letu kote ulimwenguni.
Kwa kuwa mimi ninaangalia zaidi upande wa ufundi, nichukue nafasi hii pia kuwasihi wanariadha wa hapa nchini kuanza maandalizi ya mbio hizi, maana mwezi desemba si mbali, japo najua kuwa wapo ambao walishaanza maandalizi tangu tulipozindua rasmi mwaka jana. Itakuwa si vyema nafasi za juu zikichukuliwa na wageni, wakati sisi tunao wana riadha wazuri hapa nyumbani.
Toa Maoni Yako:
0 comments: