Ama kweli dunia kuna mambo, wakati wengine wanahangaika kutafuta watoto mpaka kwa waganga wengine nao watoto hao wanawatupa, tukio hilo limetokea mjini Songea baada ya Mtoto Bahati Upendo mwenye siku 3 toka azaliwe alipo wekwa na mama yake kwenye mfuko wa mbolea na kutumbukizwa kwenye shimo, Ndani ya shimo hilo amekaa siku 6 bila kula wala kunywa hadi alipo okotwa na wasamalia wema.

Hivi sasa mtoto huyo yupo hospitali ya mkoa wa Ruvuma akiwa Salama Salimini, uongozi wa hospitali huo unaomba msaada kwa yeyote anayeweza kusaidia mtoto huyo; anaweza kwenda moja kwa moja hospitalini au wasiliana na namba zifuatayo mchango utafwatwa 0755061588 au 0755 731 234.
Waganga na maofisa wa Jeshi la Polisi wakiwa wamefika hospitalini hapo kumjulia hali. (Picha kwa hisani ya Jeshi la Polisi, Ruvuma.)
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: