Majira ya saa 2 usiku ameokotwa mtoto wa kiume anayekadiriwa kuwa na miezi mitatu karibu na kiwanda cha Bidco karibu na magorofa ya bima kando ya dimbwi la maji huku mtoto huyo akiwa hajavalishwa nguo.

Kwa mujibu wa mashuhuda waliofika eneo la tukio na kumchukua mtoto huyo na kumpeka kituo cha polisi Mikocheni 'B', jijini Dar es Salaam walisema kuwa walishangaa kusikia kilio cha mtoto mchanga ndipo waliposogea eneo la tukio na kukuta mtoto huyo akiwa eneo la tukio akiwa peke yake katupwa bila nguo.

Mashuhuda hao wamesikitishwa na kitendo hicho na kuomba jamii kuacha matendo ya unyanyasaji ambayo imekuwa ikiyafanya.
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: