Mfano halisi wa barabara ya mabasi yaendayo kasi inayoendelea kujengwa kwenye barabara ya Morogoro, katikati ni sehemu ya kituo cha abiria na mabasi ya kasi, pembeni ni barabara ya magari ya kawaida.
NIMEKUWA nikipokea maswali mengi kutoka kwa wasomaji wa blog kutaka kufahamu namna mfumo huo wa mabasi utakavyo kuwa wengi wao hasa wakiwa na hofu ya kuwepo kwa ajali nyingi kwenye barabara hiyo.
Pichani hapo juu unaonyesha mfumo huo utakavyokuwa kwenye eneo la Manzese. Mamlaka inayohusika na usimamizi wa Ujenzi huo ya DARTS wamekuwa wakitoa maelezo kwa muda mrefu hasa kwenye maonyesho mbalimbali lakini si vibaya kama nami nikiwapa somo.
Kwa mamtiki hiyo ningependa ndugu wasomaji muelewe ya kuwa mfumo huo unaonekana pichani ndiyo mfumo wenyewe utakavyokuwa, kwa maana kinachoonekana katikati ni kituo ambacho kisingi kitawahifadhi abiria wote wanaokwenda na kurudi mjini (Kariakoo, Posta na Ferry) na mabasi yaendayo kasi yatasimama kulia na kushoto mwa kituo kutegemea na liendako.
Wakazi wa jiji la Dar wakipata maelezo juu ya mfumo wa magari yaendayo kwa kasi.
Usafiri utakuwa ni bora zaidi kwa sababu abiria watalipa nauli kabla ya kupanda basi, watapumzika kwenye kituo bila ya kuunguzwa na jua na barabara ya mabasi hayo yatakuwa yakipita yenyewe tu bila kuingiliana na magari mengine na kutoa fursa ya mwendo wa kasi.
Kuhusu magari mengine kama inavyoonekana pichani pembeni kabisa kutakuwa na barabara kwajili ya magari mengine ya kawaida huku kukiwa na sehemu maalum kwaajili ya kuvuka watembea kwa miguu.
Toa Maoni Yako:
0 comments: