Tigo Tanzania imetangaza mshindi wa droo kubwa ya promosheni ya smartcard kuwa Herieth Andrew Makurukuru mkazi wa mbezi jijini Dar es Salaam

Mshindi huyo ameshinda zawadi kuu ambayo ni tiketi ya bure ya kwenda na kurudi Uingereza pamoja na kulipiwa gharama zote za safari na Tigo kwenda kushuhudia moja kwa moja Mechi kati ya Manchester United na Arsenal.

Alivyojulishwa kuhusu ushindi wake akiwa na bashasha tele, Bi Herieth Andrew Makurukuru

"Mshindi wetu atalipiwa gharama zote za safari yeye pamoja na rafiki yake mmoja na Tigo, kwenda kushuhudia moja kwa moja Mechi kati ya mahasimu wawili wa Ligi Kuu ya Barclays ya Uingereza mwezi Aprili mwaka huu. Kushinda droo hii, mashiriki anatakiwa kuwa mteja wa Tigo na mtumiaji wa simu aina ya Blackberry, Android ama I-phones," alifafanua David Sekwao, meneja Ubunifu na Ofa wa Tigo.

Droo hiyo ni mwendelezo wa droo za promosheni ya smartcard ambazo zinaendelea kufanyika kila mwezi, robo mwaka, na kila mwaka. Promosheni ya smartcard ilizinduliwa Septemba 2012 hususan kwa ajili ya wateja wa Tigo ambao wanatumia smartphones kama Blackberry, Android ama iphone

Bwana Sekwao aliendelea kwa kusema kuwa "Mbali na zawadi kuu ya droo hii, washindi 42 watabahatika kujishindia zawadi mbalimbali zikiwemo tiketi 12 za sinema, tiketi 12 za klabu, tiketi 12 za kuangalia mechi za mpira kwenye klabu ya hapa nchini, vocha 3 za kununua bidhaa mbalimbali na vocha 3 za chakula cha jioni.”

Aliongeza kuwa “mMshindi wa leo atapatiwa tiketi ya bure ya kwenda na kurudi Uingereza ambapo atalipiwa gharama zote za safari kwenda kuangalia mechi ya soka kati ya Arsenal na Manchester United ambazo ndio timu kuu za ligi kuu ya Barclays ya Uingereza.

Kushiriki katika shindano hili, mteja alitakiwa awe amejiunga na kifurushi cha Smartcard chenye thamani ya Tshs 30,000 kwa mwezi na awe ametumia huduma hii kwa miezi mitatu mfululizo na vilevile awe amejiunga na jamii ya smartcard kupitia www.tigo.co.tz/smartcardcommunity.

Zawadi nyingine kuu za mwaka za droo hii ni pamoja na tiketi ya ndege ya kwenda na kurudi Dubai, malazi ya siku 5 pamoja na hela ya matumizi kiasi cha shilingi laki moja na nusu kwa siku na vilevile tiketi na gharama za kwenda na kurudi Uingereza kuangalia mechi kati ya Arsenal na Man United mwezi Aprili mwaka huu.
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: