
Meneja Chapa ya Tigo Bw. William Mpinga akitongea na waandishi wa habari wakati wa uzinduzi wa kifurushi cha KABAANG! kulia ni Mbunifu wa ofa za Tigo Bi.Jacqueline Nnunduma.

Mbunifu
wa ofa za Tigo Bi.Jacqueline Nnunduma akifafanua jambo kwa waandishi wa
habari wakati wa uzinduzi wa bidhaa mpya ya kifurushi cha KABAANG! kwa
wateja wa mtandao wa Tigo.
---
Na Mwandishi Wetu.
Tigo
Tanzania imezindua bidhaa mpya ijulikanayo kama “KABAANG” ambayo
itawapa wateja wake fursa ya kupata muda wa maongezi wa bure, kifurushi
cha intanet na ujumbe mfupi bila kikomo kwa kujumuisha huduma hizi kuu
tatu kwenye kifurushi kimoja.
“KABAANG”
ni kifurushi cha wiki ambacho mteja akijiunga anapata dakika 300 za
muda wa maongezi ambazo anaweza kuzitumia kupiga simu kwenda mtandao
wowote ule, anapata kifurushi cha intaneti na kuweza kutuma ujumbe mfupi
bila kikomo.
”
Tuliona kuna haja kubwa sana ya kuzindua bidhaa itakayohusisha mahitaji
mbalimbali ya wateja wetu kwenye kifurushi kimoja cha bei nafuu na
kitakachowapatia wateja matumizi mbalimbali.
Kifurushi hiki cha wiki
kinamruhusu mteja kutumia huduma mchanganyiko ipasavyo na kwa bei nafuu
kabisa na kitawafaa sana wajasiriamali na waajiriwa wa mashirika
mbalimbali kwani kitawawezesha kuwasiliana kwa simu, sms na barua pepe
muda wowote wakati wakiendelea na mambo mengine kwa shilingi 9000 tu
wateja wa Tigo wanapata huduma nyingi na bora zaidi ” alisema Ndg.
William Mpinga, Meneja wa chapa ya Tigo.
Ndg.
Mpinga aliendelea kwa kusema ” kwa kutumia KABAANG wateja wetu wataweza
kuwasiliana vizuri zaidi kwani itapunguza mzigo wa uhitaji wao wa
kutaka kuwasiliana kila wakati kwani inawapatia bidhaa iliyojumuisha
mahitaji yao makuu ya mawasiliano kikazi na kwenye biashara. Mteja
anahitaji laini moja tu ya simu kufurahia bidhaa hii bora kutoka Tigo”.
Kutumia
kifurushi hiki mteja anabidi atume neno “Kabaang” kwenda 15711, na
baada ya hapo atapata ujumbe wa kuadhimisha kujiunga na kuweza kutumia
kifurushi. Kabaang inapatikana kwa wateja wote wa Tigo wenye simu
zinazotumia intaneti na kinagharimu shilingi 9,000 tu kwa wiki.


Toa Maoni Yako:
0 comments: