Aliyekuwa Mgombea wa nafasi ya
Urais wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) na baadaye kuenguliwa kugombea nafasi
hiyo na Kamati ya Rufaa ya Uchaguzi huo, Jamali Malinzi anazungumza hivi sasa
na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam kuhusiana na uamuzi huo na kusema
kuwa maamuzi hayo ameyasikia tu kwa vyombo vya Habari lakini hadi sasa hajapata
barua rasmi. Vile vile madai yaliyotolewa hadi kuenguliwa kwake sio sahihi kwani sifa zote anazo.
Wanahabari
ambao ni wapigapicha kutoka vyombo mbalimbali vya Habari vya ndani na
Kimataifa, wakichukua picha wakati Malinzi akizungumza hii leo.
Waandishi
wa vyombo mbalimbali wa habari wakimsikiliza kwa makini maelezo ya Jamali Malinzi
juu ya hatua iliyochukuliwa na Kamati ya Rufaa ya uchaguzi wa TFF chini
ya Mwenyekiti wake Idd Mtinginjola. Picha na Mroki Mroki.
Toa Maoni Yako:
0 comments: