Padre Zacharia Matilo (pichani) wa Kanisa Katoliki la jijini Nairobi, Kenya amfagilia msanii wa muziki wa kizazi kipya kwa kutumia wimbo wake katika mahubiri yake wakati ibada ya ndoa katika kanisa la Mtakatifu Petro na Paulo la Kijenge, Arusha.
Akihubiri katika ibada hiyo Padre Zacharia Matilo wikendi iliyopita alisema kuwa wanandoa wengi wamejisahau kuwa wao ni mwili mmoja kwa kujitenga ama kuficha ficha mambo yao likiwemo suala la matumizi ya simu za mkononi.
Padre huyo aliwaacha wanaumini midomo wazi pale alipoanza kuimba wimbo wa msanii wa muziki wa kizazi kipya Barnaba, usigombane kisa meseji, baby sijui amekosea namba haipaswi kulalamika, haiwezekani tumpigie weka loudspika tumpigie haiwezekani akosee namba wakati wenye simu ni wengi.
“Napenda niwaase wanandoa nyie wapya, tambueni ninyi ni mwili mmoja wala hakuna haja ya kufichana mambo yenu yasije yakawa yake yaliyoibwa katika wimbo ule unaosema, Tusigombane kisa meseji, baby sijui amekosea namba haipaswi kulalamika, haiwezekani tumpigie weka loudspika tumpigie haiwezekani akosee namba wakati wenye simu ni wengi, Aliimba Padre Matilo kwa kuwawekea msisitizo wanandoa hao wapya.
Aliongeza kuwa ndoa nyingi za sasa zimekuwa ni fasheni kwa wanandoa wengi kujisahau kwa kukosa upendo baina yao.
Jumla ya ndoa tatu zilifungwa ikiwemo ya Bw. Kennedy Angelo Kajuna na Bi. Siza Mkoma ambao wamemua kuachana na kambi ya ukapela.
mapadre nao ni binadam kwa hivyo kama muzik umemgusa hawezi kujizuia
ReplyDelete