Na Mwandishi Wetu 

MBUNGE wa Ludewa Deo Filikunjombe, kesho anatarajia kuwa mgeni rasmi katika uzinduzi wa bendi ya victoria Sound 'Wana wakawaka wazee wa gesi', utakaofanyika Kwenye Ukumbi wa Mango Garden jijini Dar es Salaam. 

Akizungumza na Kajunason Blog, kiongozi wa bendi hiyo Mwinjuma Muumini (pichani) alisema kuwa maandalizi yote yamekamilika, ikiwa ni pamoja na mbunge huyo kukubali kuwa mgeni rasmi.

 Muumin alisema kuwa wanamuziki wa bendi yake wapo tayari kutoa burudani safi katika ujio wa bendi wao mpya. Alisema kuwa katika kambi yao waliyoweka sawa kuonyesha uwezo wao katika muziki. 

Muumin alisema katika bendi yao wapo wanamuziki wapya ambao ndiyo wanaanza rasmi katika muziki ikiwa ni pamoja na wazoefu kama Waziri Sonyo.

 "Nawakaribisha mje muone mambo mapya kutoka kwa wazee wa gesi, tunakuja kivingine kabisa, tunaomba mje na kutuunga mkono" alisema Muumin.

Alisema katika uzinduzi huo watasindikizwa na kikundi cha taarab pamoja na bendi ya Extra Bongo 'Wazee wa Kizigo' chini ya Ally Choki.
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: