Captain David Nickol mzee wa karne ya sita ambaye alikuwa mkuu wa wilaya enzi za ukoloni kabla ya Tanganyika kupata uhuru mwaka 1961 akiweka shada la maua katika sanamu la askari lililopo jijini Dar es Salaam ikiwa ni ishara ya kuwakumbuka askari mashujaa waliopigana vita kuu ya pili ya dunia mwaka 1939 hadi mwaka 1945 na vita ya kumuondoa Idd Amin mwaka 1978 hadi mwaka 1979.

 Captain David Nickol mzee wa karne ya sita akitoa heshima.
Captain David Nickol mzee wa karne ya sita akitoa saruti mara baada ya kukamilisha zoezi la kuweka shada la maua.
Haya ndiyo maneno yaliyoandikwa katika sanamu hilo la askari lililopo katikati ya jiji la Dar es Salaam.
---
WATANZANIA wametakiwa kujituma katika kazi ikiwa ni pamoja na kutii mamlaka zilizopo katika serikali na hata kwenye dini, hatua ambayo itasaidia kudumisha amani na mshikamano ulioachwa na hayati mwalimu Julius Kambarage Nyerere.

Wito huo umetolewa jana na Captain David Nickol mzee wa karne ya sita ambaye alikuwa mkuu wa wilaya enzi za ukoloni kabla ya Tanganyika kupata uhuru mwaka 1961, ambapo alisema amani iliyopo nchini Tanzania ni msingi wa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere hivyo inapaswa kuenziwa.

Bw. Nickol aliyasema hayo wakati akiweka shada la maua kwenye sanamu la askari lililopo katikati ya jiji la Dar es Salaam, kuwakumbuka askari mashujaa waliopigana vita kuu ya pili ya dunia mwaka 1939 hadi mwaka 1945 na vita ya kumuondoa Idd Amin mwaka 1978 hadi mwaka 1979.

Alisema nchi ya Tanzania toka zamani imejulikana kama nchi ya utulivu na amani na kwamba Hayati Julius Kambarage Nyerere alisisitiza vitu hivyo enzi za uhai wake, hivyo ni vema watanzania wote wakasimama kupigania hilo ili kuweza kuepuka vurugu.

Bw. Nickol aliwahi kuwa mkuu wa wilaya katika maeneo mbalimbali hapa nchini enzi za ukoloni na kuhitimisha kazi hiyo mwaka 1961 wilaya ya Kisarawe mkoani Pwani ni mmoja wa wapiganaji katika vita kuu ya pili ya dunia mwaka 1939 hadi mwaka 1945.
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

1 comments:

  1. "Mzee wa Karne ya Sita"? Na tunaye miongoni mwetu hadi leo hii, katika Karne ya Ishirini-na-Moja? Kuna kitu hapo ambacho sijakielewa.

    Hata hivyo, ninatolea Mzee David Nickol heshima zote kuwakumbuka na kuwaenzi wale wote waliotoka nchini mwetu ambao alipigana nao bega kwa bega miaka hiyo ya 1939 hadi 1945.

    ReplyDelete